Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Aug 22, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_46231" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akikata utepe kuashiria uwashaji rasmi umeme katika Kijiji cha Isenegeja wilayani Igunga[/caption]

Na Hafsa Omar, Tabora

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ameendelea na ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme vijijini ili kuhakikisha kuwa lengo la Serikali la kuhakikisha kuwa vijiji vyote vinafikiwa na nishati ya umeme ifikapo mwaka 2021 linafanikiwa.

Tarehe 21 Agosti, 2019, alikagua kazi hiyo katika Kijiji cha Mwisi, Uswaya na Isenegeja wilayani Igunga ambapo..... aliwasha umeme katika Kijiji cha Isenegeja.

Aidha, akizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti, alilisisitiza kuhusu  wananchi kulipia gharama ya shilingi 27,000 tu, na bila kujali aina ya nyumba wanazomiliki.

“ Umeme ndiyo nguzo kuu ya maendeleo,  hivyo nawasisitiza kuchangamkia huduma hii inayotolewa na Serikali ili muweze kujifanyia shughuli mbalimbali za kiuchumi, kama tulivyosema umeme hautachagua nyumba, umeme wa Serikali hii unapelekwa kwa watanzania wote bila kujali masikini, tajiri au mtanzania wa kawaida.”alisema Dkt Kalemani.

Aidha, Dkt Kalemani aliwaagiza wakandarasi kuacha tabia ya kuchelewa kuwaunganishia umeme wananchi  “ nimeshasema ni marufuku kuchelewa kuunganishia umeme wananchi,  mtu akishalipia  muunganishie umeme ndani ya siku Saba bila kisingizio chochote.”

Kuhusu hali ya umeme nchini, alisema kuwa, hali ya umeme ni nzuri na endapo kunatokea kukatika kwa nishati hiyo, ni  kwasababu ya hitilafu tena ya dharura ama kwasababu ya matengenezo.

Kwa nyakati tofauti wananchi wa Vijiji hivyo waliishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kusambaza nishati ya umeme vijijini na kueleza kuwa itawawezesha kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuanzisha mashine za kukoboa nafaka ambapo hapo awali walilazimika kutumia dizeli ili kuziendesha lakini kwa sasa watatumia nishati ya umeme na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi