Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio katika picha ziara ya Makatibu Wakuu 11 Wilayani Mbarali kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji vya Wilaya hiyo
Oct 07, 2018
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_36433" align="aligncenter" width="900"] Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora (asiye na miwani) pamoja na Mabatibu Wakuu wakisikiliza maelezo ya Mtaalam kutoka Ofisi za Bonde la Maji la Mto Ruaha Bw.Idris Msuya walipotembelea katika Mfereji wa Mnazi kuona uharibifu wa uchepushaji maji katika Mto Ruaha mkuu Wilayani Mbarali Mbeya, Oktoba 06, 2018.[/caption] [caption id="attachment_36434" align="aligncenter" width="900"] Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel akiangalia mashine za Power tiller zinazotumiwa na wakulima wa mashamba ya Mpunga ya Madibira katika kuchepusha maji kutoka Ruaha walipotembelea maeneo hayo pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara 11 zinazohusika na suala la Hifadhi ya rasilimali maji na maliasili.[/caption] [caption id="attachment_36435" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Albert Chalamila akimuonesha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora uharibifu wa uchepushaji wa maji kutoka Mto Ruaha Mkuu unaofanywa na wakulima wa maeneo hayo walipofanya ziara Wilayani Mbarali Oktoba 6, 2018.[/caption] [caption id="attachment_36436" align="aligncenter" width="900"] Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel akiruka mfereji wa maji wa Mnazi unaotoa maji kutoka mto Ruaha wakati wa ziara yao katika kijiji cha Warumba kata ya Ubaruku Wilayani Mbarali Mbeya.[/caption] [caption id="attachment_36437" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Albert Chalamila akitoa maelezo kwa Makatibu Wakuu walipotembelea mashamba ya Mpunga ya mnazi katika kijiji cha Mwanavala Kata ya Imalilosongwe Wilayani Mbarali Mbeya Oktoba 06, 2018.[/caption] [caption id="attachment_36438" align="aligncenter" width="900"] Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt.Hamisi Mwinyimvua akichangia hoja wakati wa kikao cha majumuisho cha Makatibu Wakuu 11 pamoja na Watendaji wa Serikali walipokutana Wilayani Mbarali ili kujadili na kutafuta suruhu ya mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na vijiji vya Wilaya hiyo.[/caption] [caption id="attachment_36439" align="aligncenter" width="900"] Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof.Kitila Mkumbo akifafanua jambo wakati wa kikao kazi cha Makatibu Wakuu walipokutana kutafuta suruhu ya mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na vijiji vya Wilaya hiyo.[/caption] [caption id="attachment_36440" align="aligncenter" width="900"] Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel Mkumbo akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi hicho.[/caption] [caption id="attachment_36441" align="aligncenter" width="900"] Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Amoni Mpanju akichangia jambo wakati wa kikao kazi hicho.[/caption] [caption id="attachment_36432" align="alignnone" width="900"] Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi.Dorothy Mwanyika akitoa ufafanuzi wa masuala ya ardhi wakati wa kikao kazi hicho.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi