Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mhagama Atembelea Mradi wa Ujenzi Kiwanda cha Sukari Mkulazi
Oct 01, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_36081" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akisalimiana na baadhi ya watendaji alipowasili katika kiwanda cha sukari cha Mkulazi (Mbigili), Mkoani Morogoro kukagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho.[/caption]

Na: Mwandishi wetu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Mkulazi (Mbigili) Mkoani  Morogoro kujionea maendeleo ya Ujenzi wa kiwanda hicho kuelekea katika hatua ya kuanza uzalishaji.

Akizungumza katika ziara hiyo, Waziri Mhagama amewataka watendaji wa Mradi wa Ujenzi wa kiwanda hicho pamoja na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuhakikisha wanatumia mradi huo kwa manufaa ya Taifa na kuwasisitizia wafanye kazi kwa weledi ili  kuendeleza kiwanda hicho wakizingatia uadilifu katika utendaji kazi wao.

[caption id="attachment_36082" align="aligncenter" width="898"] Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. William Erio akimwelezea jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipotembelea kiwanda cha sukari cha Mkulazi kilichopo Mbigili, Mkoani Morogoro alipofanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho.[/caption] [caption id="attachment_36083" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akisisitiza jambo kwa watendaji wa kiwanda hicho na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. William Erio alipofanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho.[/caption]

"Lazima kila mmoja wenu atekeleze majukumu yake kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Serikali ili azma ya kuanzishwa kwa kiwanda hiki itimie, kwa kuwa nia ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Mhe. Rais Dkt John Magufuli ni kuhakikisha kuwa inajenga uchumi wa viwanda ambao ni jumuishi na unalenga kuwanufaisha wananchi wote na manufaa ya kiwanda hiki ni kwa wanachama". Alisisitiza Mhe Mhagama

Akifafanua Zaidi, amesema kuwa Kiwanda hicho kitakapoanza uzalishaji kitatoa ajira kwa watanzania wengi na kuchangia katika kukuza uchumi wa Taifa letu.

[caption id="attachment_36084" align="aligncenter" width="900"] Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. William Erio akisisitiza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipotembelea mashamba ya miwa ya kiwanda cha sukari cha Mkulazi kilichopo Mbigili, Mkoani Morogoro kukagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho.[/caption] [caption id="attachment_36085" align="aligncenter" width="900"] Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa katika kiwanda cha sukari cha Mkulazi Bw. Gerald Sondo akimuonesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) eneo la shamba walilopanda hekta 860 za miwa ambayo imekwa bila kutegemea umwagiliaji.[/caption] [caption id="attachment_36086" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na watendaji wa kiwanda cha Sukari cha Mkulazi kuhakikisha wanatumia mradi huu kuleta manufaa yanayotarajiwa.[/caption] [caption id="attachment_36087" align="aligncenter" width="900"] Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. William Erio akifafanua jinsi mtambo wa kuvutia maji ya kisima unakavyokuwa unafanya kazi ya umwagilia. (Katikati) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipofanya ziara ya ukaguzi katika kiwanda hicho. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu)[/caption]

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. William Erio  aliahidi kuyafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na Waziri  Mhagama na kumhakikishia  kuwa watashirikiana na Bodi ya Wadhamini ya Shirika hilo kusimamia kwa uadilifu mkubwa mradi huo.

Pia alisisistiza kuwa wataendelea kufanya juhudi kubwa katika kutekeleza mipango yote itakayowezesha kuanza mapema iwezekanavyo kwa uzalishaji wa sukari katika kiwanda hicho.

Ziara hiyo ya Waziri Mhagama ililenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa kiwanda cha Sukari cha Mkulazi pamoja na kukagau mashamba ya Miwa ya kiwanda hicho ili kujionea hatua iliyofikiwa katika kuelekea kwenye uzalishaji wa sukari na muelekeo wa uchumi wa viwanda nchini.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi