Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makatibu Wakuu, MaRAS Watakiwa Kuzingatia Taratibu, Kanuni na Sheria kwa Maendeleo ya Wananchi
Sep 19, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_35428" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi akifungua Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19,2018. (Picha na: Frank Shija - MAELEZO)[/caption]

Na: Frank Mvungi- MAELEZO

Katibu  Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi amewataka Makatibu Wakuu wa Wizara na Makatibu Tawala wa Mikoa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria , Kanuni, Taratibu na Miongozo inayotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano  kila wanapofanya maamuzi.

Akizungumza leo Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha siku tatu kwa Viongozi hao Balozi Kijazi amesema kuwa  wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanazingatia taratibu zote ili azma ya kujenga uchumi wa viwanda ifikiwe kwa wakati na kuwanufaisha wananchi.

“Nafasi zenu ni za maamuzi hivyo msipofanya maamuzi sahihi na kwa wakati mtakwamisha shughuli za maendeleo na huduma muhimu kwa wananchi.” Alisisitiza Mhandisi Kijazi.

[caption id="attachment_35420" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya washiriki wa Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu wa Wizara na Makatibu Tawala wa Mikoa wakifuatilia kikao kazi chao kinachoendelea Jijijini Dodoma.[/caption]

Akifafanua, Mhandisi Kijazi amesema kuwa wajumbe wa mkutano huo wanalojukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanafanyia kazi masuala yote yatakayoazimiwa katika kikao kazi hicho cha siku tatu kinacholenga kuongeza tija katika ngazi ya Wizara na Mikoa kwa kuzingatia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano yakuleta mageuzi makubwa katika nyanza zote hasa katika huduma zinazotolewa kwa wananchi.

[caption id="attachment_35417" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi akiwa kwenye picha ya pamoja na Makatibu Wakuu mara baada ya kufungua kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19,2018.[/caption]

Aliongeza kuwa Kikao kazi hicho kina umuhimu mkubwa na kitakuwa kikifanyika kila mwaka ili kuwapa fursa Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala  kubadilishana uzoefu, kubaini changamoto zilizopo na kuweka utaratibu mzuri wa kuzitatua kwa maslahi ya wanachi.

Akizungumzia mabadiliko yaliyofanywa na Serikali Balozi Kijazi amesema kuwa ni pamoja na kuwepo kwa muundo mpya kwa Wizara zote unaoendana na mahitaji na mipango ya Serikali ya Awamu ya Tano utakowezesha kutatutuliwa kwa changamoto zilizokuwepo kabla ikiwemo kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.

Kauli mbiu ya Kikao kazi hicho ni “Uongozi makini na wapamoja unaozingatia uzalendo, uwajibikaji, utawalabora na kusimamia rasilimali zetu ni nyenzo muhimu katika kuifikisha Tanzania katika uchumi wa Kati” Alisisitiza Balozi Mhandisi  Kijazi.

Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu wa Wizara, Makatibu Tawala wa Mikoa Kinafanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kikilenga kuimarisha na kuongeza tija katika kuwahudumia wananchi kama ilivyo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi