Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Huduma bora za upasuaji wa moyo zaifanya JKCI kutambulika kimataifa - Sheikh Chizenga
Sep 14, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_35257" align="aligncenter" width="750"] Naibu Balozi wa Saudi Arabia Mhe. Ahmed Al Ghamidi akimkabidhi zawadi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga wakati wa hafla fupi ya kuwashukuru wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchini humo walioko nchini kwa ajili ya kufanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa ambao valvu zao hazifanyi kazi vizuri. Kushoto Mwakilishi wa Mufti Sheik Hassan Chizenga.[/caption]

Na Salome Majaliwa - JKCI

Huduma bora za matibabu pamoja na upasuaji wa moyo zimeifanya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kutambulika kimataifa na hivyo wataalamu wengi kutoka nje ya nchi kuvutiwa  kwenda kufanya kambi maalum za  matibabu  ya moyo kwa kushirikiana na madaktari wa Taasisi hiyo.

Hayo yamesemwa leo na Mwakilishi wa Mufti, Sheikh Hassan Said Chizenga wakati wa hafla fupi ya kuwashukuru wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya  Misaada (IIRO) ya nchini Saudi  Arabia ambao wako JKCI  katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo.

Sheikh Chizenga alisema Taasisi ya Moyo  imekua kimbilio kwa wagonjwa wa  Afrika na Dunia nzima kwa ujumla kutokana na huduma bora za matibabu ya moyo zinazolewa  kiufanisi.

[caption id="attachment_35258" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga akimkabidhi tuzo ya kutambua kazi ya upasuaji wa moyo wanayoifanya kwa wagonjwa Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo pamoja na mishipa ya damu Khalid Kamal Alhroub kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchini Saudi Arabia ambao wako JKCI kwa ajili ya kambi maalum ya matibabu ya moyo. Hadi sasa jumla ya wagonjwa 14 wameshafanyiwa upasuaji wa moyo na kubadilishwa valvu zaidi ya mbili.[/caption]

“Taasisi hii imekua kioo si kwa Afrika tu bali Dunia nzima kwa kutoa huduma ya matibabu ya Afya ya moyo na upasuaji kwa wagonjwa ambao ni watanzania na wengine kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati” ,alisema Sheikh Chizenga.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Agnes Kuhenga aliishukuru  nchi ya Saudi Arabia kwa ushirikiano inaouonyesha kwa Serikali ya Tanzania katika kuimarisha utaalam na kuboresha utoaji wa huduma za afya hapa nchini.

“Ushirikiano wa Tanzania na Saudi Arabia umelenga kuhakikisha watanzania wanakuwa na afya bora na kuweza  kushiriki katika shughuli mbalimbali  za kiuchumi na kulifanya taifa letu kufikia lengo la kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025”, alisema Kuhenga.

[caption id="attachment_35256" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi wa Mufti Sheik Hassan Chizenga akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Balozi wa Saudi Arabia Mhe. Ahmed Al Ghamidi, viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete na wafanyakazi wa Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchini Saudi Arabia mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuwashukuru wataalam kutoka nchi hiyo ambao wako JKCI kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu ya moyo.[/caption]

Naye Naibu Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mhe. Ahmed Al Ghamidi alisema katika kambi hiyo wataalamu kutoka nchi zote mbili wameweza kuunganisha nguvu na ujuzi waliokuwa nao na kufanya matibabu kwa wagonjwa.

Mhe.Balozi Ghamidi alisema, “Katika kambi hii ya siku saba maisha ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji yameweza kuokolewa na  pindi watakapopona watarudi nyumbani na kuendelea na majukumu yao ya kazi za kila siku”,.

Katika kambi hiyo jumla ya wagonjwa 20 wanatarajia kufanyiwa  upasuaji wa moyo wa kufungua kifua na kubadilishwa   valvu zaidi ya mbili ambapo hadi leo  wagonjwa 14 walishafanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi