Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Nditiye Afungua Mkutano wa Umoja wa Taasisi za Posta wa SAPOA
Jul 10, 2018
Na Msemaji Mkuu

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi na Mawasiliano) Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia) akiwa meza kuu pamoja na baadhi ya wawakilishi wa Umoja wa Posta kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SAPOA), katika mkutano wa umoja huo, alioufungua leo, ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwan'gombe na wa pili ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo.
Baadhi ya wawakilishi kutoka DHL ambao ni wafadhili wa mkutano huo wakifuatilia maelezo mbalimbali kutoka kwa wawakilishi wa nchi mbalimbali za umoja huo.
Wawakilishi kutoka Shirika la Posta Tanzania (TPC) wakiskiliza kwa makini maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na wawakilishi wa nchi za umoja huo, wakati wa  ufunguzi wa mkutano huo. Kutoka kushoto ni Kaimu Meneja Uendeshaji wa Biashara, Mwanaisha Saidi, Kaimu Meneja Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo na Meneja Huduma za Fedha, Rehema Mbunda.
Baadhi ya wawakilishi kutoka nchi za Kusini mwa Afrika zilizounda umoja huo, wakifuatilia kwa makini hotuba na maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika mkutano huo.
                                                 Baadhi ya wawakilishi wa umoja wa SAPOA, kutoka nchi za Kusini mwa Afrika, wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
                                                               Mtendaji Mkuu wa Posta wa Mauritius, Giandev Moteea, akitoa hotuba yake katika mkutanoni huo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Posta (SAPOA), katika Ukumbi wa  Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam leo. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati), akiwa na Mtendaji Mkuu wa Posta nchini, Mauritius Giandev Moteea (wa nne kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta (TPC), Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo (wa nne kulia), Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta, Hassan Mwang'ombe (wa tatu kulia), katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi kutoka nchi mbalimbali zilizo katika Umoja wa Posta kwa nchi zilizo ya Kusini mwa Afrika (SAPOA), jijini Dar es Salaam leo. 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi