Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Neema Lowassa,(wapili kulia), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali za wanavyuo wa elimu ya juu mkoa wa Dar es Salaam, wakionyesha vipeperushi vyenye melezo ya Mfuko huo, baada ya semina ya siku moja iliyoandaliwa na PSPF kuelimisha wanafunzi shughuli mbalimbali za Mfuko na fursa zilizopo. Semina hiyo imefanyika leo Juni 8, 2017.
Na: Mwandishi Wetu
Jumla ya wawakilishi 250 wa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu kutoka jijini Dar es
Salaam wamejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wake wa
uchangiaji wa hiari (PSS), baada ya kushiriki semina ya siku moja katika makao makuu
ya Mfuko jijini Dar es Salaam Juni 8, 2017.
Wanafunzi hao kutoka Taasisi 20 za Elimu ya juu, wamehudhuria semina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na PSPF kwa uratibu wa Taasisi ya Elimu ya Vyuo Vikuu Tanzania, (TAHILISO),ili kuwapatia elimu wanafunzi hao kuhusu shughuli za Mfuko na faida anazozipata mwanachama.
Mwenyekiti wa TAHILISO, Bw.Stanslaus Peter Kadugalize,(aliyesimama), akifafanua baadhi ya mambo mwishoni mwa semina hiyo. Wengine kutoka kushoto, ni Katibu Mkuu wa TAHILISO, Bi. Zuhura A. Rashid, Afisa Mfawidhi wa PSPF mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Neema Lowassa, na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi.
Kabla ya zoezi hilo la kujiunga na Mfuko, awali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bi.
Costantina Martin, aliwaasa wanafunzi hao kujijengea utamaduni wa kuweka akiba
kwani manufaa yake huonekana katika kipindi kifupi.
“Mimi nina mtoto yuko Chuo kikuu huwa ninampatia fedha kidogo za kujikimu lakini
namueleza aweke akiba, ningependa kuwahamasisha vijana mjenge utamaduni wa kujiwekea akiba kidogo kidogo,zile posho mnazopata, na fedha kutoka kwa wazazi wenu,mnaweza kutenga sehemu ya fedha hizo na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima ilikujiwekea akiba.” Alisema Bi. Costantina Martin, wakati akifungua semina hiyo.
Alisema,
PSPF, kama Mfuko wa hifadhi ya jamii, moja ya malengo yake ni kuandikisha
wanachama wapya , kukusanya michango, kuwekeza na kuwalipa mafao na pensheni
wastaafu na wategemezi ili waweze kupata fedha kwa ajili ya matumizi yao ya
kila siku.
Katibu Mkuu wa TAHILISO, Bi.Zuhura A.Rashid, (kushoto), akijaza fomu ya kujiunga na PSPF kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS)
Viongozi wa wanafunzi wakijaza fomu za kujiunga na PSPF
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bi.Costantina Martin,akifungua semina hiyo
Aliwashauri wanafunzi hao kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari, ili hatimaye waanze kufaidi mafao mbalimbali ikiwemo faola matibabu ambapo mwanachama anapatiwa bima ya afya itakayomuwezesha kutibiwa yeye mwanachama na wategemezi wake.
Ili kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa salama, PSPF inaendesha mipango ya aina
mbalimbali ya uchangiaji, mpango wa lazima na mpango wa hiari ili kuhakikisha
kila Mtanzania anakuwa salama katika Hifadhi ya PSPF.
“Najua wataalamu wetu watawapa elimu ya kutosha kuhusu aina za wanachama kwani hata ninyi mnaweza kuwa wanachama wetu kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari PSS,ambapo mnaweza kujiunga na kupatiwa kadi zenu leo hii baada ya semina.”
Alsiema.
Afisa Mfawidhi wa PSPF Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Neema Lowassa, akizungumza kwenye senima hiyo
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, akizunguzma na baadhi ya viongozi wa wanafunzi wa elimu ya juu, walipotembelea kuona jinsi utunzaji taarifa za wanachama wa Mfuko zinavyohifadhiwa. Hii ilikuwa ni sehemu ya semina waliyopewa viongozi hao na maafsia wa PSPF jijini Juni 8, 2017
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Elimu ya Vyuo Vikuu Tanzania, (TAHILISO),Bw.Stanslaus Peter Kadugalize, ameishukuru PSPF kwa kuwa mshirika mzuri na kukubali ombi la wanafunzi hao kupatiwa elimu juu ya hifadhi wa jamii.
“Ninachoomba, PSPF inaweza kuangalia namna gani inaweza kusaidia wanafunzi
katika ushiriki wao kwenye elimu, kwa mfano mnaweza kutusaidia hata kutujengea vimbweta kwenye vyuo vyetu, lakini pia mnaweza,uwekeza kwenye ujenzi wa hosteli ambazo sisi wanafunzi tutalipa kodi.” Alsiema.
Afisa mwandamizi wa kitengo cha utunzaji kumbukumbu (record keeping), Bw. Gwamaka A. Ngomale, (mwenye kofia), akiwaeleza washiriki hao namna PSPF inavyotunza kumbukumbu kwenye mfumo wa kielektroniki wa makabati (electronic shelves)
Maafisa wa PSPF, walitoa mada mbalimbali ambazo miongoni mwake ni pamoja na Jenga Career na PSPF, ambao ni mkopo wa elimu, Jipange kimaisha na PSPF, ambapo PSPF hutoa mikopo kwa mwajiriwa mpya,
Hata hivyo wanafunzi hao waliiomba PSPF kutengeneza mfumo ambao unaweza kuwasaidia wanafunzi kuwawezesha nkushiriki kwenye elimu bila matatizo.
Wanafunzi walisema kuwa hawahitaji fedha nyingi, mnaweza kuweka mfumo utakaowawezesha wanafunzi kupata mikopo midogo ya fedha ili kuwawezesha kujikimu wawapo vyuoni na hatimaye wanafunzi hao wanaweza kurejesha fedha hizo kwa utaratibu utakaokubaliwa na pande mbili.