Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mhandisi Kamwelwe, Amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara Hiyo Kufanya Mabadiliko Makubwa ya Kiutendaji Kwenye Bohari Kuu ya Maji
Dec 07, 2017
Na Msemaji Mkuu

Na: Mwandishi Wetu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Issack Kamwelwe, amesitisha manunuzi yote ya vifaa vya maji yanayofanywa na Bohari Kuu ya Maji jijini Dar es Salaam hadi hapo Serikali itakavyoelekeza vinginevyo.
Lakini pia ameagiza mamlaka zote zinazotekeleza miradi ya maji au zinazoendesha utoaji wa huduma ya maji waende bohari kuu kuangalia vifaa vinavyoweza kutumika kwao ili wavinunue viishe kabla ya kuelekea kwenye hatua nyingine.
[caption id="" align="aligncenter" width="640"] Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Issack Kamwelwe, akiangalia dira za kupimia maji, alipotembelea bohari kuu ya maji Boko jijini Dar es Salaam, Desemba 5, 2017.[/caption]
[caption id="" align="aligncenter" width="640"] Meneja wa Bohari Kuu ya Maji Bw. Clepline Bulamo, akizungumza wakatyi akitoa taarifa kwa Mhe. Waziri Kamwelwe.[/caption]  
Kume kuwepo na ununuzi holela wa vifaa, Halmashauri na Mamlaka za maji zimekuwa zikijinunulia vifaa jinsi wanavyotaka na hii ni hatari sana ndio maana miradi mingi haiendani na thamani halisi ya vifaa, na vinapatikana kwa gharama kubwa, Alisema Mhandisi Kamwelwe.
“Mamlaka zote za maji zilizo chini ya wizara yangu, mtu asije akaenda kununua vifaa nje ya bohari kuu kama kifaa hicho kinapatikana kwenye bohari hiyo.” Alisema Mhandisi Kamwelwe.
Aidha Waziri Kamwele amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kufanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji kwenye bohari hiyo kwani kwa hali ilivyo imeshindwa kabisa kutekeleza majukumu yake.
[caption id="" align="aligncenter" width="640"] Mhe. Kamwelwe, (kushoto), akionyeshwa moja ya vifaa vya maji vinavyotunzwa kwenye bohari kuu ya maji na Meneja wa Bohari Kuu ya Maji Bw. Clepline Bulamo[/caption]
 Mhandisi Kamwelwe, (Kushoto), akizungumza jambo mbele ya Meneja wa Bohari Kuu ya Maji, Bw. Clepline Bulamo, na watendaji wakuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang'ingo, (wapili kushoto) na Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, mhandisi Mhandisi Cyprian Luhemeja, wakati wazirin akikagua vifaa vya maji vinavyotunzwa kwenye bohari hiyo, Boko jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Waziri alitoa maagizo hayo wakati alipotembelea bohari hiyo iliyoko Boko jijini Dar es Salaam, mwanzoni mwa ziara yake ya kutembelea miradi ya maji inayotekelezwa na Serikali kupitia DAWASA Desemba 5, 2017.
Alilaumu utendaji duni wa watendaji wa Bohari hiyo unaoonyesha kuishiwa ubunifu. Na hivyo kufanya shughuli kulegalega.
Mhandisi Kamwelwe, (Kushoto), akiongozana na Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mwang'ingo, wakati akikagua vifaa hivyo vya maji kwenye bohari kuu ya maji.
Mabomba ya maji yakiwa kwenye eneo la wazi kwenye bohari hiyo
[caption id="" align="aligncenter" width="640"] Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang'ingo,  (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja, wakijadili jambo wakati wa ziara ya Mheshimiwa Waziri.[/caption]
Waziri Kamwelwe, na ujumbe wake akiendelea na ukaguzi wa vifaa vya maji
[caption id="" align="aligncenter" width="640"] Waziri Kamwelwe, na akiendelea na ukaguzi wa vifaa vya maji kwenye bohari kuu ya maji, Boko jijini Dar es Salaam[/caption]
Waziri Kamwelwe, (Kulia), akiuliza jambo mbele ya Meneja wa Bohari Kuu ya Maji Bw. Clepline Bulamo Dar es Salaam.
“Serikali imenunua vifaa vyenye thamani ya shilingi bilioni 4.83 vingine vinaonekana vimepitwa na wakati, lakini vingine vinaonekana vinaweza kutumika, na bohari inahitaji watu ambao ni wabunifu, na kwa vile vilivyopitwa na wakati viko viwanda vinatengeneza vifaa kama hivyo uongozi ni bora ukawasiliana na viwanda hivyo ili waone tatizo ni nini na inawezekana kuboresha eneo ambalo linavifanya visitumike ili vikaweza kutumika na kuokoa fedha za serikali.
“Nakuagiza ufanye kazi hiyo kwa haraka na umpatie taarifa Katibu Mkuu, sitaki kuona kitu hata kimoja kinapotea kwani vifaa hivi vimenunuliwa na kodi za wananchi na fedha za serikali.” Aliagiza Waziri Kamwelwe.
Katika hatua nyingine, Waziri amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kufanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji kwenye bohari hiyo ili pawepo na wataalamu husika kuloingana na shughuli za bohari. Aidha Waziri ametoa muda wa mwezi mmoja kwa wadeni wote wa Bohari Kuu ya Maji, kulipa madeni yao vinginevyo atachukua hatua baada ya muda huo kupita.
 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi