Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

PST Yaunga Mkono Agizo la JPM Ujenzi wa Viwanda Vya Dawa
Dec 04, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_24059" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Chama cha Wafamasia Tanzania (PST) Issa Hango (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu kuunga mkono tamko la Rais John Pombe Magufuli juu ya uanzishwaji wa viwanda vya dawa nchini, kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Maadili wa chama hicho Twalib Msango na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Aggrey Dudu.[/caption]

Na: Mwandishi Wetu

CHAMA Cha Wafamasia Tanzania (PST) kimemuunga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu maelekezo yake aliyoyatoa hivi karibuni ya uwekezaji katika ujenzi wa viwanda vya dawa za binadamu pamoja na vifaa tiba nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Rais wa PST, Issa Hango alisema agizo hilo la Rais Magufuli limetoa fursa kwa Wafamasia nchini kuweza kujipanga na kuzalisha bidhaa bora zitakazoweza kukidhi mahitaji stahiki kwa wagonjwa na wananchi kwa ujumla.

[caption id="attachment_24060" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Maadili wa Chama cha Wafamasia Tanzania (PST) hicho Twalib Msango (kushoto) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu kuunga mkono tamko la Rais John Pombe Magufuli juu ya uanzishwaji wa viwanda vya dawa nchini, katikati ni Rais wa chama hicho Issa Hango na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Aggrey Dudu.[/caption] [caption id="attachment_24061" align="alignnone" width="750"] Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafamasia Tanzania (PST)Aggrey Dudu (kulia) akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu kuunga mkono tamko la Rais John Pombe Magufuli juu ya uanzishwaji wa viwanda vya dawa nchini, katikati ni Rais wa chama hicho Issa Hango na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Maadili wa chama hicho Twalib Msango. (Picha na Eliphace Marwa)[/caption]

Hango alisema uwepo wa viwanda vya utengenezaji wa dawa za binadamu nchini utasaidia kwa kiasi ubora na upatikanaji wa uhakika wa dawa, udhibiti wa utengenezaji, kutengeneza ajira na kupunguza matumizi ya pesa za kigeni katika manunuzi ya dawa hizo nje ya nchi.

Aliongeza kuwa katika kuchangamkiia fursa hiyo ya Serikali PST tayari imeandaa mapendekezo mbalimbali inayopanga kuyawasilisha Serikalini kwa ajili ya kujadiliana na mamlaka zinazohusika ili kuhakikisha kuwa wanatekeleza kwa vitendo agizo hilo lilitolewa na Rais Magufuli.

“Nitoe rai kwa Wizara, taasisi na mashirika yote yanayohusika katika kutimiza adhma hii yaweke mazingira wezeshi kwa kushirikiana na PST ambacho ni chombo rasmi kinachowaunganisha wanataaluma wote wa kada ya Famasi” alisema Hango.

Alisema ujenzi wa viwanda vipya vya dawa utasadia kwa kiasi kikubwa kuongeza uwezo wa utendaji kazi wa viwanda vilivyopo nchini ambavyo kwa sasa vinafanya kazi chini ya asilimia 35 kutokana na changamoto ya uagizaji wa madawa kutoka nje ya nchi yanayofanana na dawa zinazozalishwa na viwanda vilivyopo nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Maadili ya PST, Twalib Msangi PST imepanga kuitumia fursa hiyo kikamilifu ili kuweza kupata soko la uhakika kwa kufanya tafiti na kutathimini miradi iliyopo pamoja na mifumo ya usajili wa viwanda hivyo.

Alisema PST imedhimishwa na jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kutekeleza adhma ya uchimi wa viwanda na ajenda hiyo kwa sasa itaweza kutekelezwa kutokana na uwepo wa utashi wa kisiasa katika usimamizi wake.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi