Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Idadi ya Wachangiaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) Yaongezeka

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo jijinini Dodoma ambapo alisema wachangiaji wa mfuko huo wameongezeka kutoka wanachama 164,706 mwaka 2001/2002 hadi wanachama 873,012 septemba mwaka huu.

Mkurugenzi wa NHIF Bw.Bernad Konga akijibu maswali kutoka kwa wajumbe wa kamati ambapo alisema mfuko wake upo tayari kuanza mara moja kutoa huduma kupitia vifurushi vipya vitakavyojulikana kama JIPIMIE ili watanzania waweze kupata huduma za matibabu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akifafanua jambo mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo jijini Dodoma.

Wakurugenzi wa NHIF wakipitia taarifa ya mfuko huo wakati ikiwasilishwa kwenye kamati mapema leo

Waziri Ummy Mwalimu akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Idara Kuu Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya(mwenye miwani) na Mkurugenzi wa NHIF Bernad Konga

Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe.Peter Serukamba akichangia taarifa hiyo

Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wakimsikiliza Waziri wa Afya(hayupo pichani)akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mfuko wa bima wa NHIF(Picha zote na Wizara ya Afya)

145 thoughts on “Idadi ya Wachangiaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) Yaongezeka

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama