Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Huduma za Mafunzo kwa Wadau wa Mahakama Kusogezwa

Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akielezea jambo alipotembelea mradi wa ujenzi wa Kituo cha mafunzo kwa ajili ya wadau wa Mahakama leo Jijini Dar es Saalaam. Kituo hicho kinajengwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kitakuwa kikitumiwa na Taasisi ya Uongozi wa Mahakama (IJA) katika kutoa mafunzo kwa njia ya teknolojia ya kiasa. Kushoto kwake ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania (WB) Bi. Bella Bird na Mtaalamu wa Benki ya Dunia (WB) Bw. Waleed Malik (kulia).

Na: Frank Shija

Mahakama imeanzisha Kituo cha mafunzo kwa lengo la kusogeza huduma za mafunzo kwa wadau mbalimbali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa maboresho ya Mahakama nchini.

Hayo yamebainishwa leo na Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma alipotembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha mafunzo kinachojengwa katika Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Mpango Mkakati wa Mahakama Tanzania pamoja na Maboresho ya Huduma za Mahakama Mhe. Zahara Mruma akielezea kuhusu mradi wa ujenzi wa Kituo cha mafunzo kwa ajili ya wadau wa Mahakama leo Jijini Dar es Saalaam. Kituo hicho kinajengwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kitakuwa kikitumiwa na Taasisi ya Uongozi wa Mahakama (IJA) katika kutoa mafunzo kwa njia ya teknolojia ya kiasa. Waliokaa mbele ni Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma (kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania (WB) Bi. Bella Bird.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo Kaimu Jaji Mkuu Mhe. Profesa Ibrahim Juma amesema kuwa  kituo hicho kitasaidi sana kwa mahakimu, majaji, waendesha mashtaka, wapelelezi na wadau wengine kupata mafunzo wakiwa katika maeneo yao kwa ukaribu zaidi badala ya kusafiri hadi Chuo cha Uongozi wa Mahakama kilichopo Lushoto Tanga.

“ Tunaanzisha Kituo hiki hapa Dar es Salaam kitakachotumika kutoka mafunzo kwa Mahakimu, Wapelelezi, Majaji, wadau wetu wakiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hata nyie Waandishi wa Habari mtapata fursa hiyo,” alisema Mhe. Profesa Ibrahim.

Kwa upande wake Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia (WB) Waleed Malik amesema kuwa amefurahishwa na namna ujenzi huo unavyoendelea na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mahakama katika kutekeleza mpango mkakati wa miaka mitano wa Mahakama unaoenda sambamba na maboresho ya huduma za Mahakama.

Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akiwa pamoja na Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Wambali (kushoto kwake) Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania (WB) Bi. Bella Bird na Mtaalamu kutoka Benki hiyo Bw. Waleed Malik (kulia) wakimsikiliza mtaalamu wa teknolojia ya ujenzi ya Moladi, walipotembelea mradi wa ujenzi wa Kituo cha mafunzo kwa ajili ya wadau wa Mahakama leo Jijini Dar es Saalaam. Kituo hicho kinajengwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kitakuwa kikitumiwa na Taasisi ya Uongozi wa Mahakama (IJA) katika kutoa mafunzo kwa njia ya teknolojia ya kisasa.

Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akiwa pamoja na Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Wambali (nyuma yake) Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania (WB) Bi. Bella Bird na Mtaalamu kutoka Benki hiyo Bw. Waleed Malik (kulia) wakiangalia moja ya vifaa vinavyotumika katika ujenzi walipotembelea mradi wa ujenzi wa Kituo cha mafunzo kwa ajili ya wadau wa Mahakama leo Jijini Dar es Saalaam. Kituo hicho kinajengwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kitakuwa kikitumiwa na Taasisi ya Uongozi wa Mahakama (IJA) katika kutoa mafunzo kwa njia ya teknolojia ya kiasa.

Naye Mratibu wa mpango huo Mhe. Zahara Maruma amesema kuwa kituo hicho kitakuwa kikitumia teknolojia ya kisasa katika utoaji wa mafunzo kupitia njia ya video conference ambapo wawezeshaji watatumia kituo hicho kuwasiliana moja kwa moja na wanafunzi wakiwa katika maeneo yao.

Mhe. Zahara amesema kuwa lengo kubwa la Mahakama ni kuunganisha Mahakama zote katika mfumo wa video conference ambazo zitawezesha watumishi kupata mafunzo wakiwa katika maeneo yao ya kazi.

Aliongeza kuwa kukamilika kwa kituo hicho kusaidia katika kutunza muda, na gharama zilizokuwa zinatumiwa kwa ajili ya mafunzo kwa kuwa watumiaji wa mahakama watapata huduma hiyo wakiwa katika maeneo yao ambapo Mahakama zao zitakuwa na mtandao wa video.

Baadhi ya mafundi wakiendelea na ujenzi mradi wa Kituo cha mafunzo kwa ajili ya wadau wa Mahakama leo Jijini Dar es Saalaam. Kituo hicho kinajengwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kitakuwa kikitumiwa na Taasisi ya Uongozi wa Mahakama (IJA) katika kutoa mafunzo kwa njia ya teknolojia ya kiasa.

Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi Mahakama na Benki ya Dunia (WB) walipotembelea mradi wa ujenzi wa Kituo cha mafunzo kwa ajili ya wadau wa Mahakama leo Jijini Dar es Saalaam. Kituo hicho kinajengwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kitakuwa kikitumiwa na Taasisi ya Uongozi wa Mahakama (IJA) katika kutoa mafunzo kwa njia ya teknolojia ya kiasa. Kutoka kushoto ni Mtaalamu kutoka Benki hiyo Bw. Waleed Malik, Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Wambali na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania (WB) Bi. Bella Bird na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Beatrice Mutungi.  (Picha zote na: Idara ya Habari – MAELEZO)

“ Mfumo huu utaondoa ulazima kwa majaji na wadau kwenda Lushoto kwa ajili ya mafunzo badala yake watapata mafunzo kupitia mtandao wa Video Conference wakiwa maeneo yao moja kwa moja kutoa hapa au Lushoto” alisema Mhe. Zahara.

“Kukamilika kwa Kituo hiki kutatoa fursa kwa uanzishwaji wa vituo vingine kama hiki katika maeneo mengine ya hasa katika Mahakama Kuu za Kanda,” aliongeza.

Ujenzi wa kituo hiki unagharimu jumla ya shilingi milioni 78 chini ya ufadhiri wa Benki ya Dunia ambapo ujenzi wake utachukua muda wa wiki nane kutokana na kutumia teknolojia ya kisasa ya ujenzi nafuu ijulikanyo kama Moladi. Kituo hiki kitakuwa kikitumiwa na Taasisi ya Uongozi wa Mahakama (IJA) kilichopo Lushoto katika kutoa mafunzo kwa wadau wa Mahakama.

65 thoughts on “Huduma za Mafunzo kwa Wadau wa Mahakama Kusogezwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama