Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Halmashauri Jiji la Arusha Kuanzisha Mahakama ya Jiji

Na Fatuma S. Ibrahimu – Arusha Jiji

Halmashauri ya Jiji la Arusha imetenga kiasi cha Shilingi milioni 20 kwa ajili ya kuanzisha mahakama ya Jiji ifikapo Tarehe 20 mwezi Novemba mwaka huu.

Ujenzi wa mahakama hiyo ni kwa lengo la kushughulikia kesi mbalimbali za wafanyabiashara wataokaidi kulipa kodi ya Serikali au ushuru wa vibanda vya biashara zao kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza na leo Jijini Arusha Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maulid Madeni amesema kuwa kuanzishwa kwa mahakama hiyo kutasaidia kuongeza mapato katika Halmashauri kwa kuwa jiji tayari zipo sheria ndogo zitakazotusaidia kupitisha hukumu kwa watakaopatikana na hatia ya ukoseshaji wa mapato ya Halmashauri.

“Katika Mahakama itakayoanzishwa tutaweza kutoa hukumu kwa masaa machache ikiwa ni faini ama kifungo kwa wataopatikana na hatia ya kuinyima mapato halmashauri, itasaidia mapato ya jiji kuongezeka na itamsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kutekeleza ahadi zake kwa watanzania ikiwa ni pamoja na huduma bora za afya na elimu kwa kupitia mapato yatakayopatika” alisema Dkt. Madeni.

Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Kalist Lazaro ameunga mkono juhudi za serikali ya awamu hii katika ukusanyaji wa mapato na ameahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa Mkurugenzi katika operesheni yake ya ukusanyaji wa mapato.

“Kamwe asijitokeze wananchi yoyote kukwepa kulipa kodi ama ushuru kwa mwamvuli wa chama fulani cha siasa , katika suala la mapato tuondoe itikadi zetu za vyama ili Halmashauri iende mbele” alisema Mhe. Kalist.

Pia aliongeza kwa kusema kuwa operesheni maalum ya ukusanyaji wa mapato bado inaendelea ili kufikia malengo ya ukusanyaji wa shilingi Bilioni 30 kwa mwaka badala ya bilioni 15 tunazokusanya sasa.

One thought on “Halmashauri Jiji la Arusha Kuanzisha Mahakama ya Jiji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama