Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Dkt. Shein Kuwapongeza Wanafunzi Waliofaulu Mitihani ya Taifa.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati alipokuwa akiwapongeza Wanafunzi waliofaulu Mitihani ya Taifa ya kidato cha Nne na Sita pamoja kuwaalika chakula cha mchana katika hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuwapongeza Wanafunzi waliofaulu Mitihani ya Taifa ya kidato cha Nne na Sita pamoja kuwaandalia chakula cha mchana katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.

Mwaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliohudhuria katika hafla ya kuwapongeza Wanafunzi waliofaulu Mitihani ya Taifa ya kidato cha Nne na Sita pamoja na kuwaandalia chakula cha mchana, hafla iliyotayarishwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimzawadia mwanafunzi Wahda Mbarak Uzia wa Skuli ya Sekondari ya Fedha katika hafla ya kuwapongeza Wanafunzi waliofaulu Mitihani ya Taifa ya kidato cha Nne na Sita pamoja kuwaandalia chakula cha mchana katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar, ,kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe.Riziki Pambe Juma.

Baadhi ya wanafunzi wakichukua chakula katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi waliofaulu Mitihani ya Taifa ya kidato cha Nne na Sita iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.

140 thoughts on “Dkt. Shein Kuwapongeza Wanafunzi Waliofaulu Mitihani ya Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama