Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Dkt.Shein Akuatana na Ujumbe wa Benki ya CRDB.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipokea Hundi ya Shilingi za Kitanzania Milioni Ishirini na kutoka kwa Mkurugenzi Masoko wa Benki ya CRDB, Bi.Tully Esther Mwambapa zilizoahidiwa na Benki hiyo kwa ajili ya mchango wa madawati kwa Shule za Serikali sambamba na kupokea milioni tano kwa ajili ya Ujenzi katika Shule ya chekechea Madungu Wilaya ya Chakechake Pemba, ujumbe wa Benki hiyo ulipofika Ikulu Mjini Unguja leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na ujumbe wa Benki ya CRDB unaoongozwa na Mkurugenzi Masoko Bw.Tully Esther Mwambapa (wa pili kulia) ulipofika Ikulu Mjini Unguja leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na mgeni wake Mkurugenzi Masoko wa Benki ya CRDB Bi.Tully Esther Mwambapa baada ya mazungumzo na Ujumbe wa Benki hiyo ulipofika Ikulu Mjini Unguja leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Mkurugenzi Masoko wa Benki ya CRDB Bi.Tully Esther Mwambapa baada ya mazungumzo alipofika Ikulu Mjini Unguja leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao, [Picha na Ikulu – Zanzibar, 09 /11/2017.].

79 thoughts on “Dkt.Shein Akuatana na Ujumbe wa Benki ya CRDB.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama