Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Dkt. Ndungulile Atoa Mwezi Mmoja Chuo cha Ustawi kutatua changamoto Zake

Na. Immaculate Makilika

Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto  Dkt. Faustine Ndugulile  amekitaka Chuo cha Ustawi wa Jamii kutatua changamoto zake ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

Hayo yamesemwa  leo Chuoni hapo alipokuwa akizungumza na menejimenti, wafanyakazi pamoja na viongozi wa  Serikali ya wanafunzi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, ambapo pamoja na mambo mengine alisomewa taarifa ya maendeleo ya taasisi na mipango ya baadae.

“Nimesikia taarifa nzuri ya maendeleo na mafanikio pamoja na changamoto za Taasisi, nawaagiza viongozi kutatua changamoto ambazo ziko ndani ya uwezo wenu kwa kipindi cha mwezi mmoja na sisi kama serikali tutazifanyia kazi zile zinazotuhusu. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa huduma zinaendelea kutolewa kwa ubora na maslahi ya watumishi yanaboreshwa”. Alisema Dkt. Ndugulile.

Pia, Naibu waziri huyo alisema  kuwa  anataka akabidhiwe  ripoti ya utekelezaji wa utatuzi wa changamoto hizo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, kwa vile baadhi ya mambo yanahitaji ufumbuzi wa mapema ili kuboresha mazingira ya utoaji huduma katika hiyo ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii.

Aidha, ziara hiyo ya Dkt. Ndungulie katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii ni miongoni mwa ziara za  kutembelea taasisi zilizo chini ya wizara yake katika kuboresha utendaji kazi.

Ambapo, katika kuhitimisha mkutano wake na uongozi, wafanyakazi pamoja na serikali ya wanafunzi wa Taasisi, Dkt. Ndugulile alipongeza kazi nzuri inayofanywa na watumishi na aliahidi wizara kuendelea kushirikiana na Taasisi ya Ustawi wa jamii katika kutoa huduma bora zinazokidhi mahitaji ya wananchi.

105 thoughts on “Dkt. Ndungulile Atoa Mwezi Mmoja Chuo cha Ustawi kutatua changamoto Zake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama