Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Dkt. Nchemba: Serikali Imesikia Kilio cha Wananchi Kuhusu Tozo za Miamala ya Simu

Na Benny Mwaipaja,Dar es Salaam

Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema Serikali imesikia kilio na maoni ya wananchikuhusu tozo mpya ya miamala ya simu na kuwaomba wawe watulivu wakati jambo hilo linatafutiwa ufumbuzi.

Dkt. Nchemba ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari akiambatana na Waziri wa Teknolojia ha Habari na Mawasiliano Dkt. Faustine Ndugulile.

“Kwa maaneo ambayo wananchi wametoa ushauri na kuelezea namna ambavyo jambo hili linawagusa lakini pia tumepokea maeneo ambayo yanatakiwa kutoa elimu zaidi ili kujenga uelewa wa pamoja ikiwa ni pamoja na viwango vinavyokatwa kwa nayetuma na anayetoa lakini pia kuhusu mantiki ya jambo lenyewe” alisema Mhe. Mwigulu

4 thoughts on “Dkt. Nchemba: Serikali Imesikia Kilio cha Wananchi Kuhusu Tozo za Miamala ya Simu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama