Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Dkt. Kigwangalla Aendelea na Mazoezi MOI, Atembea Umbali wa Km 4

Waziri wa Maliasiali na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (Kulia) akiteta na Wasaidizi wake jana usiku katika viunga vya Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akifanya mazoezi ya kutembea ambapo alitembea umbali wa Kilometa nne. Wengine ni wasaidizi wake (kushoto) ni Katibu wa Waziri Ephraim Mwangomo na katikati ni Ramadhan Magumba.

Na Andrew Chale, Dar

Hali ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla anayepatiwa matibabu na Madaktari Bingwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu, Ubongo na Uti wa Mgongo Muhimbili (MOI), imeendelea kuimarika zaidi ambapo kwa sasa ameweza kufanya mazoezi ya kutembea umbali wa Kilometa 4 kwa kutumia muda wa saa moja na dakika 23.

Dkt. Kigwangalla ameweza kufanya zoezi hilo jana jioni  kutembea umbali huo wa Kilometa 4 na  kisha kupanda jengo la MOI kwa kutumia ngazi kutoka chini mpaka gorofa ya Sita.

“Kwa sasa naendelea vizuri. tofauti na awali nilipokuwa natembea umbali mdogo kutoka Wodi ya Mwaisela nilipokuwa nimelazwa na kutembea mpaka geti la kuingilia Hospitali hii ya Muhimbili. Kwa sasa natembea umbali mrefu zaidi, nilianza na Kilometa moja, nikaongeza kilometa  moja na nusu na baadae mbili leo nikaona niongeze zaidi na kuweza kumaliza Kilometa hizi nne.”alisema Kigwangalla.

Mazoezi haya ya kutembea yananisaidia kuimarisha zaidi mapafu ila kwa sasa bado nashughulikia mkono pekee”. Kigwangalla aliongeza.

Dkt. Kigwangalla uanza kufanya mazoezi hayo kila siku kuanzia majira ya jioni kwa lengo la kiafya pamoja na tiba kwa hali yake hiyo ambayo kwa sasa akiendelea na matibabu.

Kwa upande wa Madaktari wa MOI wamebainisha kuwa licha ya kuendelea vizuri, bado wanafuatilia kwa ukaribu hali ya afya yake hadi watakapojiridhisha ndipo watamruhusu kurejea nyumbani kuendelea na majukumu yake.

Dkt. Kigwangalla aliletwa MOI tangu Agosti 12, mwaka huu na kufanyiwa upasuaji wa mkono wake ambao ulivunjika kutokana na ajali aliyoipata Agosti 4, akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Manyara.

87 thoughts on “Dkt. Kigwangalla Aendelea na Mazoezi MOI, Atembea Umbali wa Km 4

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama