Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Dkt.Abbasi Awapa Kongole wanahabari wanaoripoti mkutano wa SADC.

Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi akizungumza na Waandjshi wa Habari (Hawapo Pichani), Kuhusu ratiba na Matukio muhimu kuelekea Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Nchi za kusini mwa Afrika-SADC katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.

Na.Mwandishi Wetu-MAELEZO.

Mkurugenzi wa Idara ya habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi, amewapongeza wanahabari wote wanaoripoti shughuli mbalimbali za mikutano ya wiki ya SADC kuanzia ufunguzi , wiki ya viwanda na hata mikutano ya ndani inayoendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Dkt.Abbasi amesema tangu kufunguliwa kwa mikutano ya SADC wanahabari wamekua mstari wa mbele kuuhabarisha umma juu ya matukio mbalimbali yanayoendelea, lakini pia kufanya shughuli za mikutano zinazoendelea zifahamike kwa umma wa watanzania.

“Nitakua mchoyo wa fadhila kama sitatambua mchango wenu kwa jinsi mnavyojitoa kufanya kazi kwa weledi lakini pia kwa uzalendo mkubwa na mapenzi kwa nchi yenu, hii inaonyesha jinsi watanzania tulivyo wamoja na makini hasa yanapokuja masuala muhimu ya kitaifa” Alisema Dkt.Abbasi.

Amesema japo mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali haujafanyika, kazi kubwa zimefanywa na wanahabari kuanzia wiki ya viwanda hadi leo ambapo Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.Palamagamba Kabudi amekabidhiwa uenyekiti wa baraza la Mawaziri la SADC.

Kwakutambua kazi nzuri inayofanywa na wanahabari, Dkt Abbasi amesema wataandaa tuzo kwa wanahabari hao baada ya kumalizika kwa mkutano Mkuu wa 39 wa nchi za SADC ili kuwapa motisha na pia kutambua mchango wao walioutoa kwa nchi.

Wakati huo huo Dkt.Abbasi amesema kwa mara ya kwanza mabalozi 42 wanaoiwakilisha Tanzania kwenye nchi mbalimbali Duniani tarehe 15 Agosti 2019 watatembelea mradi mkubwa na wa kihistoria wa kufua umeme katika maporomoko ya mto Rufiji ambao kwa sasa utajulikana kama JK Nyerere Hydroelectric Power Project.

Amesema uamuzi wa mabalozi wote kuja kutembelea mradi huo wa kihistoria ni miongoni mwa mikakati ya Serikali ya kuhakikisha wanawatumia mabalozi katika kuendeleza diplomasia ya uchumi lakini pia kutangaza mambo makubwa yanayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Mkutano wa 39 wa wakuu wan chi za SADC unatarajia kufikia kilele tarehe 17 na 18 Jijini Dar es Salaam ambapo wakuu wa nchi serikali pamoja na Wafalme kutoka katika nchi wanachama wanatarajiwa kuhudhuria.

170 thoughts on “Dkt.Abbasi Awapa Kongole wanahabari wanaoripoti mkutano wa SADC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama