Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Dkt. Abbasi Akutana na Afisa Ubalozi wa China, Akabidhiwa Vifaa

Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan Abbasi akipokea sehemu ya vitendea kazi vilivyotolewa na Ubalozi wa China hapanchini kupitia kwa Afisa Mwandamizi wa Ubalozi huo, Xu Chen mara baada ya kumalizika kwa kikao baina yao kiliofanyika leo Mei 31, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan Abbasi akisaini mkataba ya makabidhiano ya vitendea kazi mbalimbali zikiwemo kamera na drones kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi wa Idara hiyo. Makabidhiano hayo yalifanyika mara baada ya kumaliza kwa kikao baina yake na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa China, Xu Chen (kulia) kilichofanyika leo Alhamisi Mei 31, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan Abbasi akisisitiza jambo wakati alipokutana na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa China nchini Tanzania, Xu Chen  leo Alhamisi Mei 31, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Rodney Thadeus akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi ((katikati) na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa China, Xu Chen uliofanyika leo Alhamisi Mei 31, 2018 Jijini Dar es Salaam.

249 thoughts on “Dkt. Abbasi Akutana na Afisa Ubalozi wa China, Akabidhiwa Vifaa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama