Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Dk. Shein Akutana na Bodi za Wakurugenzi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) mara alipoingia katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu Mjini Unguja leo, wakati wa kikao cha siku moja kilichojumuisha Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Barabara na Uongozi wa Mfuko wa Barabara, kilichozungumzia masuala mbali mbali ya kiutendaji.

Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee (kulia) akiwa na Viongozi mbali mbali wakati wa kikao cha siku moja kilichojumuisha Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Barabara na Uongozi wa Mfuko wa Barabara kilichofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo chini ya Mwenyekiti, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Barabara Bw. Mwalimu Haji Ameir (kulia) alipokuwa akitoa maelezo ya Bodi yake kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati wa kikao cha siku moja kilichojumuisha Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Barabara na Uongozi wa Mfuko wa Barabara kilichofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,(kushoto) Mkurugenzi Mtendaji Mwalimu Ali Mwalimu (kushoto).

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Ndg. Ali Khamis (kulia) alipokuwa akifafanua jambo wakati wa kikao cha siku moja kilichojumuisha Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Barabara na Uongozi wa Mfuko wa Barabara kilichofanyika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Khali Salum Mohamed (kushoto). (Picha na Ikulu)

One thought on “Dk. Shein Akutana na Bodi za Wakurugenzi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama