Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Jamii Yatakiwa Kuyatunza Mazingira Kulinda Ardhioevu.

Tanzania ni moja wapo ya nchi zenye utajiri mkubwa wa ardhioevu na viumbe mbalimbali vinavyoishi kwa kutegemea utajiri huo,  hivyo jamii imetakiwa kuyatunza mazingira ili kuulinda utajiri huu adhimu na adimu.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Kijiji cha Makumbusho, Dkt. Gwakisa Kamatula kwenye maadhimisho ya wiki ya ardhioevu duniani yaliyofanyika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam kwa kushirikiana na ofisi ya Makamu wa Rais nchini.

Matukio katika Picha Bungeni

Bilioni 7.5 Kuimarisha Mawasiliano Nchini

Na Mwandishi Maalum – DODOMA

Serikali imelipa shilingi bilioni 7.5 kwa wakandarasi wazawa kwa lengo la kuimarisha mawasiliano nchini kujenga kilomita 409 za mkongo wa Taifa ambao kwasasa una jumla ya kilomita 7,910 huku sehemu nyingine ya fedha hizo ikitumika kwenye mradi wa anuani za makazi na postikodi kwenye Halmashauri 12.

JPM AMTANGAZA JAJI GALEBA KUWA SHUJAA WA KISWAHILI KATIKA SHERIA

JPM AMTANGAZA JAJI GALEBA KUWA SHUJAA WA KISWAHILI KATIKA SHERIA

“Tusione aibu katika kutumia lugha ya Kiswahili leo nampongeza na kumteua  Jaji wa mahakama  ya Kanda ya Mara,  Jaji Zepharine Nyalugenda Galeba kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania kwa kutumia lugha ya Kiswahili katika kutoa hukumu ya kesi Namba 23 ya mwaka 2020” Rais Magufuli.

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema “ Tunashindwa kukitumia Kiswahili kwa sababu  za kukosa utashi na ujasiri lakini pia ni ishara na kasumba ya kupenda vitu vya nje na kudharau vya kwetu kwa msingi huo nimeamua kumteua Mhe. Jaji Galeba Ujaji wa Mahakama wa Rufaa kutokana na uthubutu na ujasiri aliyoonyesha ya kuandika hukumu kwa lugha ya Kiswahili”

Urasimishaji wawezesha wananchi Njombe kukopa bilioni 3.1/-

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA), Mhe. Balozi (Mstaafu) Daniel Ole Njoolay akieleza faida za urasimishaji kwa wananchi wa halmashauri ya mji wa Njombe walionufaika na mpango huo  Januari 29, 2021 wakati wa ziara ya Kamati hiyo na Menejimenti ya MKURABITA wilayani humo kujionea maendeleo yaliyofikiwa na wanufaika hao.

Na Mwandishi  Wetu- Njombe

Wafanyabiashara na wakulima waliorasimisha biashara, ardhi na makazi yao katika Halamashauri ya Mji wa Njombe, wametumia hati za hakimili za kimila kukopa zaidi ya Shilingi bilioni 3.1 katika taasisi za fedha zikiwemo benki za NBC, CRDB, NMB na Benki ya Posta kufikia mwaka 2020.

ULEGA Aagiza Serikali za Mitaa Kutobadilisha Matumizi ya Viwanja vya Michezo

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Abdallah Ulega akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya msingi manyinga baada ya kuwapa mipira kwa ajlli ya maendeleo ya michezo katika shule hiyo.

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Abdallah Ulega ameagiza viongozi walioko Serikali za mitaa kutobadili matumizi ya viwanja vya michezo.

Waziri Ulega amesema hayo wakati alipofanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya michezo katika mkoa wa Morogoro.

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Abdallah Ulega akicheza mchezo wa Table Tennis wakati alipotembelea Shule ya sekondari  Morogoro kukagua shughuli za michezo.

“Viwanja vyote vilivyo katika ngazi ya vijiji viheshimiwe na vilindwe ili kuhakikisha vijana na watoto wanapata nafasi ya kucheza ili kuibua vipaji”aliongeza Ulega

Wakulima watumia hatimiliki za kimila kukopa benki bilioni 18.9

Mmoja wa Wakulima wa mpunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya  walionufaika na urasimishaji ardhi Bw. Paulinus Msigwa akionesha   Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) manufaa alliyopata  ikiwemo matrekta aliyonunua baada ya kurasimisha mashamba yake na kupatiwa hatimilki za kimila za kumiliki ardhi. Kamati hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Balozi (Mstaafu) Daniel Ole Njoolay imewatembelea baadhi ya wanufaika wa mpango wilayani humo.

Na Mwandishi Wetu- Mbarali

Majaliwa: Wamachinga ni Muhimu Katika Kukuza Pato la Taifa

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa Waziri Mkuu amesema Wamachinga ni watu muhimu katika kukuza pato la Taifa na takwimu za Wizara ya Viwanda na Biashara zinaonesha kuwa Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo imetengeneza ajira, kukuza uchumi na kuondoa umasikini.

Hivyo, Waziri Mkuu ameziagiza mamlaka zinazohusika na ujenzi wa masoko mazuri unaoendelea kwenye maeneo mbalimbali nchini wazingatie na waandae miundombinu kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Januari 28, 2021) katika kikao na Viongozi wa Wamachinga Tanzania katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Sekta hiyo ina jumla ya wajasiriamali milioni 3.1 ambao wameajiriwa ni asilimia 23.4 ya nguvu kazi ya Taifa na imechangia asilimia 27 katika pato la Taifa.

Kauli Mbiu ya Mkutano huo inasema “Wamachinga ni fursa sahihi ya kujenga uchumi”, ambapo, Waziri Mkuu amesema utekelezaji wake utakuwa ni muarobaini wa changamoto zote zinazowakabili Wamachinga nchini kwani kila mmoja kwa nafasi yake atatimiza wajibu wake ili kuhakikisha wanafanya kazi zao na hivyo kuweza kuchangia ujenzi wa uchumi wa Taifa.

ev eşyası depolama