Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

MOI Yaanzisha Huduma ya Upasuaji wa Ubongo na Mgongo KCMC

Madaktari bingwa wa upasuaji wa ubongo, mgongo na Mishipa ya fahamu wa MOI wakishirikiana na madaktari bingwa wa KCMC kufanya upasuaji wa uti wa mgongo katika hospitali ya KCMC, huduma hiyo imaenza ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kusogeza huduma kwa wananchi. 

Mwandishi wetu  – MOI

Taasisi ya Mifupa MOI kwa kushirikiana na Hospitali ya rufaa ya kanda ya kaskazini (KCMC) tarehe 05/02/2020 zimeanzisha ushirikiano wa kutoa  huduma za kibingwa za upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu kwa wakazi wa kanda ya kaskazini ili kuwaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu kuafuata huduma hizo Dar es Salaam au kwenda nje ya nchi.

Serengeti Festival Yaanza kwa Full Shangwe Dodoma, Show Kamili Leo, Wasanii 70+ Jukwaa Moja

Na mwandishi wetu, Dodoma

Kama uko Dodoma, Iringa, Singida, Manyara, Morogoro au hata Dar maana Shabiby lipo hadi saa tisa alasiri kama hautafika Dodoma leo usinilaumu!!!!

Sasaaaa, sikiliza jana usiku wa kuamkia leo Jumamosi Februari 6, 2021, dunia ilisimama, burudani ilitambulishwa na wanaojua burudani waliburudika.

Hiyo ilikuwa show kabla ya shughuli yenyewe leo (kwa lugha ya Shilole wanaita Serengeti Royal Pre-Party), ambapo wasanii 10 tu, kati ya zaidi ya 70 watakaotumbuiza leo, jana walitoa burudani ya kipato cha kati.

Serikali Kupitia Upya Kanuni za Uvuvi

Na Mbaraka Kambona, Dodoma

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema kufuatia changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa marekebisho ya kanuni za uvuvi za mwaka 2020, serikali imeazimia kuzipitia upya ili ziendane na mahitaji ya sasa.

Ndaki aliyasema hayo Februari 4, 2021 jijini Dodoma wakati akiongea na Waandishi wa Habari na kutoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya zana za uvuvi katika maji yote nchini.

Alisema hivi karibuni Wizara imepokea maoni na changamoto mbalimbali kutoka kwa wadau wa sekta ya uvuvi kutoka Ukanda wa Bahari, Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria kuhusiana na marekebisho ya kanuni ya uvuvi ya mwaka 2020 katika baadhi ya vipengele.

Mhagama Aridhishwa na Utendaji TACAIDS

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akieleza jambo kwa wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Dawa za Kulevya wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati Februari 4, 2021 Bungeni   Jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu- Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,Vijana ,Ajira na Wenye Ulemavu  Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI zimeendelea kuimarika hapa nchini.

Mhe. Bashungwa: Wizara inaendelea Kuratibu na Kusimamia kazi za Ubunifu

Na Shamimu Nyaki – WHUSM,Dodoma

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema Wizara inaendelea kusimamia  na kuratibu vyema shughuli za ubunifu kwa vijana kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla.

Mhe. Bashungwa ameyasema hayo Februari 04, 2021 alipokua akifungua Kongamano la I HAVE A DREAM  kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu vilivyopo Mkoa wa Dodoma lililofanyika ukumbi wa Royal Village Jijini Dodoma  ikiwa ni kuelekea Tamasha la Serengeti Music Festival ambalo kilele chake ni Fabruari 06, 2021 Uwanja wa Jamhuri jijini hapo.

Magereza Yaweza kuwa Ndio Taasisi ya Kusambaza Mbegu Tanzania Nzima – Rais Magufuli

Na Mwandishi Wetu – DODOMA

Jeshi la Magereza nchini huenda ikawa ndio Taasisi ya kusambaza mbegu nchini hivyo kupunguza gharama ya kuagiza mbegu kutoka nje ya nchi.

Hayo yamesemwa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwenye uzinduzi wa majengo ya Ofisi Kuu ya Jeshi la Magereza iliyopo Msalato jijini Dodoma.

“Mna mradi wa kuzalisha mbegu pamoja na shamba la michikichi, Magereza inaweza ikawa ndio Taasisi ya kusambaza mbegu Tanzania nzima, litakuwa jambo zuri kwa sababu mbegu zitakuwa ni zetu tofauti na za kuletewa ambazo ukizipanda zinaweza zisiote” ameeleza Mheshimiwa Rais

Rais wa Zanzibar, Dkt Mwinyi Azungumza na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala Ikulu Leo.

Waziri Mkuu Atoa Siku Tatu Ripoti ya Watumishi Wanaoishi Nje ya Vituo Vyao Imfikie

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameipa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ifuatilie Halmashauri zilizopaswa kuhamia kwenye maeneo yake na impatie taarifa ifikapo Jumamosi, Februari 6, 2021.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Februari 4, 2021) wakati akijibu swali la mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu bungeni jijini Dodoma.

Mbunge huyo alitaka kujua Serikali inatoa kauli gani kuhusu watumishi hao walioshindwa kutii agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa Oktoba 24, 2019 akiwataka wahamie kwenye makao makuu ya Halmashauri zao kabla ya Oktoba 30, 2019.

Bw. Musukuma amesema kitendo hicho kinaitia Serikali hasara kwani watumishi hao walihamisha ofisi tu kwenda makao makuu ya Halmashauri lakini wanaendelea kuishi mijini.

Rais Magufuli Afungua Majengo ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza pamoja na Miradi Mingine ya Jeshi hilo Mkoani Dodoma

Jamii Yatakiwa Kuyatunza Mazingira Kulinda Ardhioevu.

Tanzania ni moja wapo ya nchi zenye utajiri mkubwa wa ardhioevu na viumbe mbalimbali vinavyoishi kwa kutegemea utajiri huo,  hivyo jamii imetakiwa kuyatunza mazingira ili kuulinda utajiri huu adhimu na adimu.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Kijiji cha Makumbusho, Dkt. Gwakisa Kamatula kwenye maadhimisho ya wiki ya ardhioevu duniani yaliyofanyika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam kwa kushirikiana na ofisi ya Makamu wa Rais nchini.

ev eşyası depolama