Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Bungeni Leo katika Picha

Mbunge wa Jimbo la Buyungu Mhe. Mhandisi Christopher Chiza akiapa mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job NdugaiS leo Jijini Dodoma mara baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Mbunge wa Kibakwe Mhe. George Simbachawene akisisitiza kuhusu faida za Dodoma kuwa makao makuu ya nchi yetu leo Bungeni Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akisisitiza jambo wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni jijini Dodoma.

Sehemu ya wabunge wakifuatilia mkutano wa 12 kikao cha kwanza cha Bunge leo Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akijibu swali Bungeni Kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuwezesha mikoa kutekeleza miradi ya kimkakati ya maendeleo ili kuinua uchumi wa mikoa hiyo.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimpongeza mbunge wa Buyungu Mhe. Mhandisi Christopher Chiza mara baada ya kula kiapo mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai leo Bungeni Jijini Dodoma.

2 thoughts on “Bungeni Leo katika Picha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama