Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Asali ya Tanzania Yazidi Kupata Soko

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Mhandisi Christopher Chiza (wakwanza kushoto) akionja asali inayozalishwa Tanzania wakati wa siku ya asali iliyoadhimishwa leo ikiwa ni sehemu ya maonesho ya Kimataifa ya 41 biashara ya Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu JK Nyerere ,barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE Bw. Edwin Rutageruka.

Na. Frank Mvungi

Wazalishaji wa asali nchini wametakiwa kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi ambalo limeendelea kukua na kuchochea maendeleo ya sekta hiyo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekitiwa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Mhandisi Christopher Chizawa wakati akifungua maonesho ya siku ya asali yaliyoafanyika leo katika viwanja vya Mwalimu JK Nyerere, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Maonesho ya Kimataifaya Dar es Salaam (Sabasaba).

“Kila mwaka tunapeleka asali nje ya nchi hasa Ujerumani na hatujawahi kupata malalamiko kutoka huko ambako kuna maabaraza kisasa za kupima ubora wa asali na matokeo yamekuwa yakionyesha asali yetu ina ubora unaotakiwa hali inayochochea mahitaji ya asali kutoka Tanzania kwenda Ulaya na sehemu mbalimbali kuwa makubwa”, alisisitiza Mhe. Chiza

Mwenyekiti wa Bodi alieleza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwaTaasisi zote zinazo husika na sekta ya asali na mazao ya misitu zinasimamiwa vyema ili ziendelee kutoa matokeo chanya yatakayo changia katika kukuza uchumi wan chi na kuwakwamua wazalishaji wa asali.

Pia aliwataka wazalishaji wa asali kuweka mkazo katika kuongeza uzalishaji unaendana na mahitaji ya soko la Kimataifa kwa kuwa mahitaji ya asali toka Tanzania ni mkubwa hali inayo toa chanagamoto kwa wazalishaji kuongeza kasi ya uzalishaji huku wakizingatia ubora unaotakiwa katika soko.

Msimamizi wa mradi kutoka kampuni ya Central Park Bees Bi Sophia Chilambo akionesha moja ya mizinga ya kisasa inayotumika katika ufugaji wa nyuki wakati wa siku ya asali.

Kwaupande wake Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Bw. Zawadi Mbwambo amesema kuwa wakala huo unaendelea kusimamia sekta hiyo ili kuhakikisha kuwa inakuwa salama na inatoa matokeo tarajiwa katika uchumi hasa kuchochea ujenzi wa viwanda vya kusindika asali hapa nchini.

Aliongeza kuwa ufugaji wa nyuki una gharama nafuu ambazo kila mwananchi anaweza kumudu katika mazingira yake na hivyo kukuza kipato chake na kuchangia katika kuchochea maendeleo kwa kuzalisha ajira na kuongeza fedha za kigeni hapa nchini.

Baadhi ya wananchi waliofika katika banda la asali wakitazama asali inayozalishwa na wajasiriamali wa Tanzania.
(Picha na Frank Mvungi-Maelezo)

Kwa upande wake mmoja wa wajasiriamali wanaozalisha asali kutokaKikundi cha mama wawili product amesema wanaipongeza Serikali kwa juhudi inazochukua katika kuwainua wajasirimali wanaozalisha asali hapa nchini kwa kuwawezesha kushiriki maonesho ya 41 Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) na kuongeza kuwa asali ya Tanzania inakubalika kimataifa kwa ubora wake hivyo changamoto iliyopo ni kuongeza uzalishaji.

Siku ya asali Iimeadhimishwa leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Maonesho ya Kimataifa ya Biasharaya Dar es Salaam yaliyoanza June 28 hadi Julai 13 mwaka huu baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutoa agizo katika halfa ya ufunguzi wa maonesho hayo kuwa muda wa maonesho uongezwe kwa siku tano zaidi.

 

8 thoughts on “Asali ya Tanzania Yazidi Kupata Soko

 • August 11, 2020 at 5:32 am
  Permalink

  It’s very straightforward to find out any matter on net as compared to books,
  as I found this article at this website.

  Reply
 • August 11, 2020 at 7:00 pm
  Permalink

  Hi everyone, it’s my first go to see at this web site,
  and piece of writing is really fruitful in favor of me,
  keep up posting these types of articles.

  Reply
 • August 13, 2020 at 11:35 pm
  Permalink

  Hey! This post could not be written any better! Reading through this post reminds me of my previous room mate!

  He always kept talking about this. I will forward this page to him.
  Fairly certain he will have a good read. Thank you for sharing!

  Reply
 • August 25, 2020 at 12:19 am
  Permalink

  I was more than happy to discover this great site.
  I need to to thank you for ones time for this particularly fantastic read!!
  I definitely enjoyed every part of it and i also have you book-marked to see new
  information on your website. cheap flights 2CSYEon

  Reply
 • August 26, 2020 at 9:29 am
  Permalink

  Hey I know this is off topic but I was wondering if you knew of any widgets I
  could add to my blog that automatically tweet my newest twitter updates.

  I’ve been looking for a plug-in like this for quite some time and
  was hoping maybe you would have some experience with
  something like this. Please let me know if you run into
  anything. I truly enjoy reading your blog and I look forward to your new updates.

  Reply
 • September 5, 2020 at 9:53 am
  Permalink

  What’s Going down i am new to this, I stumbled upon this I’ve discovered It
  absolutely helpful and it has helped me out loads.

  I hope to give a contribution & aid other users like its aided me.

  Great job.

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama