Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Amani Na Usalama Nchini Kuimarishwa

Na, Adelina Johnbosco, MAELEZO, Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa  amewatoa hofu wananchi kwa kusema kuwa  hali ya usalama nchini imeendelea kuwa shwari.

Akiongea wakati wa kuahirisha mkutano wa kumi na nne wa bunge la kumi na moja Jijini Dodoma Mh. Majaliwa amesema kuwa wananchi wanaendelea kufanya shughuli zao mbalimbali za kiuchumi kwa utulivu na bila ya bughudha yoyote.

‘’Jambo la msingi katika kipindi hiki ni kwamba kila mmoja wetu adumishe hali ya ulinzi na usalama katika eneo alipo’’ amesema Majaliwa

Licha ya hali ya usalama kuendelea kuwa shwari, Mheshimiwa Majaliwa amelaani vikali matukio ya kinyama dhidi ya watoto Mkoni Njombe na amewaonya wale wote wenye kujaribu kutumia matukio hayo kuzui taharuki kwa jamii.

“Nitumie fursa hii kusisitiza kwamba serikali haitafumbia macho vitendo hivyo vya kikatili dhiti ya watoto wetu” Mhe. Majaliwa

Aidha, Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa ametoa pole kwa Wananchi Nchini Kenya kufuatia  tendo la kigaidi lililotokesa mnamo tarehe 15 , Januari , 2019 katika hoteli ya kifahari ya Dusit 2 Jijini Nairobi ambalo lililogharimu maisha ya watu na mali.

‘’Naomba nitumie fursa hii kuungana na Mh. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na watanzania wenzangu kuwapa pole majirani zetu Wakenya kufuatia tukio hilo baya ambalo linapaswa kulaaniwa na kila mpenda amani duniani kote’’

Vile vile, Waziri Majaliwa amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Jumuiya za Kimataifa katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Katika kuhakikisha hilo, amebainisha vyombo vya ulinzi na usalama nchini jinsi vinavyo chukua tahadhari kubwa dhidi ya vitisho vya matukio ya kigaidi ikiwa ni pamoja na kuongeza na kuongeza umakini katika kuwachuja wageni wanaoingia nchini ili kuhakikisha wanakidhi vigezo vyote vya kiusalama vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria.

Pamoja na hayo,Mheshimiwa Majaliwa amesema, mambo mengine ya kulinda amani ni utoaji elimu kwa umma juu ya manufaa ya uzalendo na kutunza amani, utayari wa vyombo vya ulinzi na usalama na kuimarisha ushirikiano nan chi jirani kikanda na kimataifa.

“Tumeendelea kubadilishana uzoefu wa udumishaji amani na nchi rafiki pamoja na taarifa za kiintelijensia kuhusu ugaidi”

103 thoughts on “Amani Na Usalama Nchini Kuimarishwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama