Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Ufunguzi wa Kongamano la Biashara Tanzania na Uganda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni, pamoja na Mawaziri wa Tanzania na Uganda wakiwa katika ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli akisisitiza Jambo mbele ya wafanyabiashara kutoka Tanzania na Uganda wakati wa Hotuba yake katika ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni akisisitiza Jambo mbele ya wafanyabiashara kutoka Tanzania na Uganda wakati wa Hotuba yake katika ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Prof.Palamagamba Kabudi akitoa maelezo ya Wizara yake mbele ya wafanyabiashara kutoka Tanzania na Uganda, wakati wa ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa akitoa maelezo ya Wizara yake mbele ya wafanyabiashara kutoka Tanzania na Uganda, wakati wa ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Prof.Palamagamba Kabudi na Waziri wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Viwanda wa Uganda, Vicent Bamulangaki wakionesha nakala za mkataba wa makubaliono kwenye sekta ya kilimo, Shughuli hiyo ilifanyika katika ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

52 thoughts on “Matukio Katika Picha Ufunguzi wa Kongamano la Biashara Tanzania na Uganda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama