Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mabondia Wawa Kivutio Bungeni Leo

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa 16 wa Bunge jijini Dodoma leo tarehe 4 Septemba 2019.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akitoa taarifa ya Serikali kukabidhi Hotuba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati wa Mkutano wa 39 SADC kwa Ofisi ya Bungeni leo jijini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa rai kwa watanzania kuiunga mkono Timu ya Taifa inayocheza leo dhidi ya Burundi wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa 16 wa Bunge jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula akijibu swali katika kikao cha pili cha Mkutano wa 16 wa Bunge leo jijini Dodoma.

Naibu wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Mhe. Juliana Shonza akijibu swali wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa 16 wa Bunge leo tarehe 4 Septemba 2019 jijini Dodoma.

Naibu wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akijibu swali wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa 16 wa Bunge leo tarehe 4 Septemba 2019 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe akijibu swali wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa 16 wa Bunge leo tarehe 4 Septemba 2019 jijini Dodoma.

Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko(kulia) na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde wakisoma kitabu cha Hotuba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati wa Mkutano wa 39 SADC ambapo Serikali imekabidhi nakala 400 za vitabu vya hotuba hiyo Bungeni jijini Dodoma leo tarehe 4 Septemba 2019.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo toka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Yusuph Singo akisalimiana na mabondia waliotembelea Bungeni kwa mwaliko maalum wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe katika kikao cha pili cha Mkutano wa 16 wa Bunge leo jinini Dodoma.

Bondia Abdallah Shabani maarufu Dullah Mbabe akipunga mikono alipokuwa akitambulishwa Bungeni leo jijini Dodoma. Bondia huyo ameibuka mshindi wa Dunia katika mchezo wa ngumi za kulipwa na kushinda mkanda wa WBO uzito wa kilo 76 dhidi ya Bondi kutoka China katika pambano lililochezwa nchini humo hivi karibuni.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimpongeza Bondia Shaban Ramadhan maarufu kama Dullah Mbabe alipotembelea Bungeni leo tarehe 4 Septemba 2019 jijini Dodoma. Bondia huyo ameibuka mshindi wa Dunia katika mchezo wa ngumi za kulipwa na kushinda mkanda wa WBO uzito wa kilo 76 dhidi ya Bondi kutoka China katika pambano lililochezwa nchini humo hivi karibuni. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana Shonza.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiangalia mkanda wa ubingwa wa dunia wa ngumi za kulipwa waWBO aliokabidhiwa Bondia Mtanzania, Abdallah Shaban aka Dullah Mbabe alipotembelea Bungeni leo tarehe 4 Septemba 2019 jijini Dodoma. Bondia huyo ameibuka mshindi wa Dunia katika mchezo wa ngumi za kulipwa na kushinda mkanda huo katika pambano la uzito wa kilo 76 dhidi ya Bondia kutoka China pambano lililochezwa nchini humo hivi karibuni. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana Shonza na Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania, Joe Anea (wapili kushoto).

Mbunge wa Kuteuliwa, Mhe. Salma Kikwete(katikati) na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kamisheni ya Ngumi Tanzania na Mabondia walioshinda mapambano ya kimataifa walipotembelea Bungeni leo tarehe 4 Septemba 2019 jijini Dodoma. Mabondia hao kulia ni Abdallah Shaban aka Dulla Mbabe bingwa wa dunia aliyeshinda mkanda wa WBO, Maono Ally aliyeshinda mkanda wa WBC na Bruno Tarimo aka Vifua viwili aliyeshinda mkanda mkanda wa IBF Intertional.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (watatu kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kamisheni ya Ngumi Tanzania na Mabondia walioshinda mapambano ya kimataifa walipotembelea Bungeni leo tarehe 4 Septemba 2019 jijini Dodoma. Mabondia hao kutoka kulia ni Abdallah Shaban aka Dulla Mbabe bingwa wa dunia aliyeshinda mkanda wa WBO, Maono Ally aliyeshinda mkanda wa WBC na Bruno Tarimo aka Vifua viwili aliyeshinda mkanda mkanda wa IBF Intertional.(Picha na Idara ya Habari – MAELEZO)

310 thoughts on “Mabondia Wawa Kivutio Bungeni Leo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama