Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Naibu Waziri Mavunde Aahidi Ushirikiano Baina ya Ofisi Yake na CBE Katika Kukuza Ujuzi kwa Vijana

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akihutubia alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 53 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) leo jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya akizungumza alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi katika mahafali ya 53 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) leo jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Ushauri la Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dkt. Esther Ishengoma akizungumza katika mahafali ya 53 ya CBE leo jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akiteta jambo na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa. Emmanuel Mjema wakati wa mahafali ya 53 ya Chuo hicho leo jijini Dodoma.

Kutoka kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde,Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Ushauri la Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dkt. Esther Ishengoma na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa. Emmanuel Mjema wakimtazama mwanamke aliyekuwa akionyesha kipaji chake wakati wa mahafali ya 53 ya Chuo hicho leo jijini Dodoma.

Mwanadada akionyesha kipaji chake cha kuchezea mpira katika mahafali ya 53 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) leo jijini Dodoma.

Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya Uhasibu wakifurahia burudani kutoka kwa mwanadada aliyekuwa akionyesha kipaji cha kuchezea mpira katika mahafali ya 53 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) leo jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akimkabidhi zawadi mmoja ya wanafunzi aliyeongoza katika taaluma alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 53 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) leo jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akitoa tamko la kuwatunuku wahitimu wa ngazi Astashahada, Stashahada na Shada katika fani za Uhasibu, Biashara, Masoko na Ununuzi toka Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 53 ya Chuo hicho leo jijini Dodoma.

Baadhi ya wahitimu wakitunukiwa shahada zao wakati wa mahafali ya 53 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) leo jijini Dodoma. (Na: Mpiga Picha Wetu).

395 thoughts on “Naibu Waziri Mavunde Aahidi Ushirikiano Baina ya Ofisi Yake na CBE Katika Kukuza Ujuzi kwa Vijana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama