Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Taarifa kwa Umma

UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI WA MAMLAKA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI – TAWA

Kufuatia uamuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, wa kumteua Meja Jenerali (Mstaafu) Hamisi R. Semfuko kuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyamapori Tanzania – TAWA, Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dkt. Hamisi A. Kigwangalla (Mb.), amefanya uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya TAWA kama ifuatavyo:

  • James V. Wakibara
  • Fredy S. Manongi
  • Robert C. Mande
  • Bi Sauda K. Msemo
  • Luteni Kanali Christian A. Ng’habi
  • Andrew M. Komba
  • CP Suzan S. Kaganda
  • Fabian M. Madele
  • Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA (Dkt. Allan J.H. Kijazi)
  • Mkurugenzi wa Wanyamapori (Kwa mujibu wa Sheria)

Uteuzi huu ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 26 Oktoba, 2018.

Prof. Adolf F. Mkenda

KATIBU MKUU

04 Novemba, 2018

One thought on “Taarifa kwa Umma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama