Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Washindi wa Multichoice Talent Factory Watakiwa Kujifunza kwa Ustadi Uandaaji wa Filamu

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na washindi wanne wa Multichoice Talent Factory (Hawapo katika picha) alipokutana nao leo katika Ofisi za Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Jijini Dar es salaam .

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (Kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) leo Jijini Dar es Salaam walipokutana na washindi wa Multichoice Talent Factory.

Na Lorietha Laurence-Dar es Salaam

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka washindi wanne wa Multichoice Talent Factory kuwa mabalozi wazuri kwa kujifunza kwa umakini yale yote watakayofundishwa katika chuo cha Sanaa Jijini Nairobi nchini Kenya.

Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokutana na Washindi hao ambao waliongozana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo ambaye amekuwa mstari wa mbele kusimamia ubora wa filamu nchini kwa kutoa mafunzo mbalimbali kwa wanatasnia hao.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na mmoja kati ya washindi wanne wa Multichoice Talent Factory Bi. Jane Moshi (kulia) alipokutana nao leo katika Ofisi za Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Jijini Dar es salaam .

“Nafasi hii ni  muhimu kwenu na kwa taifa kwa ujumla hivyo mwende mkawe mabalozi kwa kujifunza kwa ustadi mzuri ambao utaleta mabadiliko katika tasnia hii ya filamu nchini” amesema Dkt. Mwakyembe

Aidha aliongeza kwa kuipongeza Kampuni ya Multichoice Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika kuchangia ukuaji wa sekta ya filamu pamoja na  sekta ya michezo na kuwataka wadau wengine kujitokeza kwa wingi ili kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na mmoja kati ya washindi wanne wa Multichoice Talent Factory Bw. Wilson Nkya (kulia) alipokutana nao leo katika Ofisi za Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Jijini Dar es Salaam .

Kwa Upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo amewataka washiriki hao kuhakikisha wanajifunza mambo yote muhimu ikiwemo uaandaji wa miswada, uongozaji, uigizaji, cinematographer na matumizi ya vifaa mbalimbali vya kisasa vya filamu.

Naye Afisa Uhusino wa Multichoice Tanzania Bi. Grace Mgaya amewataka washiriki hao kuzingatia nidhamu ya hali juu katika kipindi chote watakachokuwa katika mafunzo  na kuitendea haki nafasi waliyopewa.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe( Katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wanne wa Multichoice Talent Factory alipokutana nao leo katika Ofisi za Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Jijini Dar es salaam . (Picha na Lorietha Laurence-WHUSM, Dar es Salaam)

Mashindano haya yalizinduliwa rasmi mwezi Mei ,2017  Jijini  Dodoma ambapo Waziri wa Habari Dkt. Harrison Mawkyembe alikuwa mgeni rasmi, ambapo wanatsnia  zaidi  165 walituma maombi kwa ajili ya kushindania nafasi hiyo, huku wasiriki 13 walipata nafasi ya kuhojiwa na baadaye kupatikana washindi wanne ambao ni wanatarajia kuijunga na chuo hicho cha Sanaa.

 Washindi hao ni  Jane Moshi kutoka Kilimanjaro, Jamal Kishuli kutoka Arusha, Sarah Kimario Kutoka Dar es Salaam na Wilson Nkya kutoka Kigoma , wanatarajia kuondoka nchini tarehe 6 Oktoba 2017 tayari kwa ajili ya kujiunga na chuo cha Sanaa Jijini Nairobi nchini Kenya .

 

183 thoughts on “Washindi wa Multichoice Talent Factory Watakiwa Kujifunza kwa Ustadi Uandaaji wa Filamu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama