Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Miss Journalism Tanzania 2018 Ateuliwa Kuwa Balozi wa Utalii Pori la Akiba Selous

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akizungumza na Miss Journalism Tanzania, 2018, Witness Teddy Kavumo
(21) ambaye pia ni mshindi wa mwaka jana wa mataji manne ya Uanamitindo nchini
Afrika ya Kusini, alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma mwishoni mwa wiki
kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki mashindano ya Dunia ya Miss Journalism
yatakayofanyika Jijini Arusha mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha, amemteua mwanamitindo
huyo kuwa balozi wa utalii wa Pori la Akiba Selous.
Na Hamza Temba-WMU
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.
Hamisi Kigwangalla amemteua mshindi wa taji la Miss Journalism Tanzania, 2018,
Witness Teddy Kavumo (21) kuwa balozi wa utalii wa Pori la Akiba Selous.
Amefanya uteuzi huo mwishoni mwa wiki
Jijini Dodoma baada ya mazungumzo na mwanamitindo huyo aliyemtembelea ofisini
kwake kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kuandaa  mradi wa kijamii ambao ni
sehemu ya shindano atakaloshiriki la taji la Dunia la Miss Journalism 2018
litakalofanyika Oktoba 27 Jijini Arusha.
Kufuatia uteuzi huo, Dk. Kigwangalla
amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi kuandika
barua ya uteuzi kwa balozi huyo mpya sambamba na kumkabidhi hati ya uteuzi ili
pamoja na mambo mengine aweze kunadi vivutio vya utalii vya pori hilo.
Wakati huo huo, Dk. Kigwangalla
amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania
TAWA, Dk. James Wakibara kuandaa safari maalum ya balozi huyo mteule aweze
kutembelea Pori la Akiba Selous kwa ajili ya kuona na kujifunza mambo mbalimbali
yanayohusu hifadhi hiyo kwa ajili ya utangazaji.
Sambamba na pori hilo atatembelea pia
mapori mengine ikiwemo BBK (Burigi, Biharamulo na Kimisi) mkoani Kagera na
Mpanga Kipengele mkoani Njombe ambapo  atatumia fursa hiyo kufanya
mahojiano na wasichana wa vijiji jirani na hifadhi hizo kwa ajili ya mradi wa
kijamii wa kuwainua ikiwa ni sehemu yenye alama muhimu kwenye shindano hilo la
Dunia la Miss Journalism 2018.
Awali akiwasilisha ombi lake kwa
Waziri Kigwangalla la ufadhili wa safari yake ya ushiriki wa mashindano hayo,
Witness pia aliomba kupewa fursa ya kuwa balozi wa Tanzania kwenye moja ya
sekta ikiwemo Misitu, Nyuki au Utalii.
Mbali na kushikilia taji la Miss
Journalism Tanzania 2018, Witness amesema amewahi kushinda mataji mengine manne
makubwa ya kimataifa ya ulimbwende nchini Afrika ya Kusini anakosomea urubani
kwa sasa.
Anasema, “Miongoni mwa mataji
hayo ni Miss Garden Route 2017, ambalo ni taji la kitaifa la kuhamasisha na
kukuza sekta ya Maliasili na Utalii nchini humo, licha ya kuwa ugenini
nilitumia fursa hiyo kunadi vivutio vya utalii vya Tanzania. 
“Mashindano haya yalihusisha
washiriki 600 na wote walikuwa na asili ya kizungu, mimi peke yangu nilikuwa na
asili ya kiafrika na niliibuka mshindi”. 
Aliyataja mataji mengine kuwa ni Miss
Bees Cape Town 2017 kwa ajili kuhamasisha uhifadhi wa sekta ya nyuki na mataji
mawili ya kimkoa ambayo ni Miss Asla Capetown 2017 na Miss Carnival Mosselbay
2017.
Mataji mengine ya kitaifa aliyowahi
kushinda Witness hapa nchini ni pamoja na Miss Arusha Higher Learning 2014 na
Miss Northern Zone 2014.
Mashindano hayo ya Dunia ya Miss
Journalism 2018 yanahusisha pia uhamasishaji wa maendeleo ya utalii, utamaduni
wa amani, uandishi wa habari na kupiga vita ugonjwa wa ukimwi na Malaria.
Pori la akiba Selous ndio hifadhi
kubwa kuliko zote nchini ikiwa na ukubwa wa kilomita za mraba takriban 50,000
katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara na Ruvuma. Mwaka 1982, Shirika
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Uneso) lilitangaza eneo
hilo kuwa moja ya eneo la Urithi wa Dunia na kuanza kuhifadhiwa.
 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja na Miss Journalism Tanzania, 2018,
Witness Teddy Kavumo (21) ambaye pia ni mshindi wa mwaka jana wa mataji manne
ya Uanamitindo nchini Afrika ya Kusini, alipomtembelea ofisini kwake Jijini
Dodoma mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki mashindano
ya Dunia Miss Journalism yatakayofanyika Jinini Arusha mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha,
amemteua mwanamitindo huyo kuwa balozi wa vivutio vya utalii vya Pori la Akiba
Selous.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla akiagana na Miss Journalism Tanzania, 2018, Witness Teddy Kavumo
(21) ambaye pia ni mshindi wa mwaka jana wa mataji manne ya Uanamitindo nchini
Afrika ya Kusini, baada ya mazungumzo ofisini kwake Jijini Dodoma alipomtembelea
mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki mashindano ya Dunia
ya Miss Journalism yatakayofanyika Jinini Arusha mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha,
amemteua mwanamitindo huyo kuwa balozi wa wa utalii wa Pori la Akiba Selous. 

 

 

 

104 thoughts on “Miss Journalism Tanzania 2018 Ateuliwa Kuwa Balozi wa Utalii Pori la Akiba Selous

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama