Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

ZiaraYa Majaliwa Wilayani Ruangwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Walimu na baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi za wilaya ya Ruangwa kwenye ukumbi wa Narung’ombe, Novemba 18, 2018. Kulia ni Mkewe Mary, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Ngandirwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi khanga Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Mkowe wilayani Ruangwa, Grace Nanguka ikiwa ni zawadi ya watumishi wote wa Kituo hicho wakati alipokagua ujenzi na ukarabati wa Kituo hicho, Novemba 18, 2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Bibi Niachia Kalembo kutoka kijiji cha Mtimbo wilayani Nachingwea ambaye ni mmoja wa wazazi waliojifungua katika Kituo cha Afya cha Mkowe wilayani Ruangwa wakati alipotembelea kituo hicho, Novemba 18, 2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mtambo wa utakatishaji vifaa vya upasuaji katika Kituo cha Afya cha Mkowe wilayani Ruangwa, Novemba 18, 2011.

 

Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akikagua ujenzi wa Gereza la Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi Novemba 18, 2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Nyumba za makazi ya askari Magereza wakati alipokagua ujenzi wa Gereza la Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi Novemba 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

46 thoughts on “ZiaraYa Majaliwa Wilayani Ruangwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *