Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Ziara ya Waziri Mkuu Majaliwa Wilayani Dodoma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Ofisi Kuu ya Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha Makutupora jijini Dodoma, Oktoba 21, 2018. Watatu kushoto ni Mkuu wa Kikosi, Luteni Jenerali Regina Matina, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge, kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde na wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kufungua ofisi kuu ya Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha Makutupora jijini Dodoma Oktoba 21, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge, kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa na wapili kushoto ni Mkuu wa Kikosi, Luteni Kanali Regina Matina.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu uzalishaji wa mvinyo kutoka kwa Bw. Archard Kato ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha Alko Vintage cha jijini Dodoma wakati alipokitembelea kiwanda hicho, Oktoba 21, 2018. Alikuwa katika ziara ya wilaya ya Dodoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi (aliyeshika kinasa sauti) kuhusu ujenzi wa soko kuu la jiji hilo kwenye eneo la Nzuguni, Oktoba 21, 2018.

Mafundi wa Kampuni ya Ujezi ya Mohammed Builders wakijenga msingi wa kituo kikuu cha mabasi kinachojengwa na jiji la Dodoma katika eneo la Nzuguni wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipoembelea eneo hilo, Oktoba 21, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi (kulia) kuhusu michoro ya stendi kuu ya mabasi inayojengwa na jiji la Dodoma katika eneo la Nzuguni, Oktoba 21, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua Mradi wa Maji wa Njedengwa wilayani Dodoma akiwa katika ziara ya wilaya ya Dodoma, Oktoba 21, 2018. Wengine pichani kutoka kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge, Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasha mashine ya kusukuma maji wakati alipofungua mradi wa maji wa Njedengwa akiwa katika ziara ya wilaya ya Dodoma, Oktoba 21, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya (wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi (kulia) kuelekea kwenye jengo la Mama na Mtoto wakati alipotembelea hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Oktoba 21, 2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma baada ya kukagua ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika hospitali hiyo, Oktoba 21, 2018. Alikuwa katika ziara ya wilaya ya Dodoma.

6 thoughts on “Ziara ya Waziri Mkuu Majaliwa Wilayani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *