Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Wilayani Serengeti

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wenza wa askari magereza wa gereza la Tabora Moja baada ya kukagua mradi wa ufugaji ng’ombe wa nyama na maziwa katika gereza hilo na kuzungumza na askari Januari 18, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia mkono wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja wa Mbuzi katika mji mdogo wa Mugumu kuhutubia mkutano wa hadhara Januari 18, 2018.Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Serengeti, Cha Marwa katika mkutano wa hadhara alipohutubia kwenye uwanja wa Mbuzi katika mji mdogo wa Mugumu wilayani Serengeti Januari 18, 2018.

Wananchi wa mji mdogo wa wilaya ya Serengeti wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mbuzi katika mji mdogo wa Mugumu Januari 18, 2018.

94 thoughts on “Ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Wilayani Serengeti

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *