Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Ziara ya Waziri Majaliwa Kongwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mhandisi wa maji Wilaya Kongwa Kaitaba Lugakingira, wakati akimuonesha kisima cha maji kwenye mradi wa maji wa Kongwa mkoani Dodoma, Oktoba 11, 2018.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua ujenzi wa daraja kwenye barabara ya Mbande – Kongwa mkoani Dodoma, Oktoba 11, 2018.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi wa Kata ya Mbande wilayani Kongwa Dodoma, aliposimama njiani na kuzungumza nao, Oktoba 11, 2018.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua majengo ya mradi wa machinjio ya kuku wilayani Kongwa Dodoma, Oktoba 11, 2018

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mashine za kukamulia mafuta ya alizeti, wakati alipotembelea kiwanda cha Com Food Products kilichopo wilayani Kongwa Dodoma, Oktoba 11, 2018.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail