Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Ziara ya Majaliwa Wilayani Bahi, Azungumza na Watumishi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo, Oktoba 19, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua daraja la Chipanga wilayani Bahi, Oktoba 19, 2018. Wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Bilinith Mahenge, Wanne kushoto ni Mbunge wa Bahi, Omary Badwel na wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Athumani.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Bahi, Kassim Kolowa (kushoto) kuhusu vifaa vilivyopo kwenye chumba cha upasuaji cha kituo hicho wakati alipokitembelea, Oktoba 19, 2018. Wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Athumani.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bibi Subi Mchome, ambaye ni mmoja wa wazazi waliojifungua salama katika wodi ya wazazi ya Kituo cha Afya cha Bahi mkoani Dodoma, Oktoba 19, 2018. Wapili kushoto ni Mganga Mkuu wa Kituo hicho, Kassim Kolowa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mtalaam wa Maabara, Petronila Olomi (kushoto) wakati alipotembealea Maabara ya Kituo cha Afya cha Bahi mkoani Dodoma, Oktoba 19, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) , Selemani Jafo na Wapili kushoto ni Mganga Mkuu wa Kituo hicho, Kassim Kolowa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka katika moja kati ya nyumba sita za walimu alizozikagua katika Shule ya Sekondari ya Mpalanga wilayani Bahi, Oktoba 19, 2019. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Athumani.

99 thoughts on “Ziara ya Majaliwa Wilayani Bahi, Azungumza na Watumishi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *