Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Zaidi ya Watanzania Milioni 12 Waishio Vijijini Wafikiwa na Huduma za Mawasiliano

  • Zaidi ya watanzania milioni 12 waishio vijijini wafikiwa na huduma za mawasiliano
  • UCSAF yatakiwa kutumia Teknolojia rahisi kufikisha huduma za mawasiliano
  • Waziri aagiza TCRA na UCSAF kushirikiana ili kuongeza kasi ya kupeleka huduma za mawasiliano vijijini

Na Celina Mwakabwale, UCSAF

Mtendaji Mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF), Justina Mashiba amesema mpaka sasa zaidi ya wananchi millioni 12 waishio maeneo ya vijijini na yasiyo na mvuto wa kibiashara pamoja na wale wa mipakani na kanda maalum wamefikiwa na huduma mbalimbali za mawasiliano ikiwemo simu, runinga, radio pamoja na mawasiliano ya posta.

Bi. Mashiba ameyasema hayo wakati wa ziara ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile aliyetembelea tasisisi hiyo na kufanya kikao na wajumbe wa bodi, menejimenti pamoja na wafanyakazi. Katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mkuu, Dkt. Zainab Chaula, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Jim Yohazi pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara hiyo.

11 thoughts on “Zaidi ya Watanzania Milioni 12 Waishio Vijijini Wafikiwa na Huduma za Mawasiliano

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama