Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Zabuni Mradi wa Umeme Rufiji zafunguliw

Wataalam kutoka Idara ya Manunuzi, Wizara ya Nishati wakifungua nyaraka mbalimbali za zabuni katika kikao hicho kilichofanyika Wizarani leo Jijini Dar es Salaam.

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

Zabuni kwa ajili ya mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme wa Megawati 2100 katika Maporomoko ya Maji ya Mto Rufiji zimefunguliwa  leo tarehe 02 Februari, 2018.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa zabuni hizo kwenye Ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi kutoka Wizara ya Nishati, Amon MacAchayo amesema zabuni hizo ni za Awamu ya Pili kutokana na kukosekana kwa mshindi katika Awamu ya Kwanza iliyotangazwa mapema mwaka jana.

Alisema kuwa, katika awamu ya kwanza jumla ya kampuni 81 zilinunua nyaraka za zabuni ambapo nakala moja ilikuwa inauzwa kwa shilingi 200,000 lakini ni kampuni nne tu zilifanikiwa kurejesha maombi na kuongeza kuwa kampuni zote nne hazikuwa na  vigezo vinavyohitajika hali iliyopelekea kutangazwa upya kwa zabuni tarehe 19 Desemba, 2017 katika vyombo vya habari  vya ndani na nje ya nchi.

Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi kutoka Wizara ya Nishati, Amon MacAchayo (mbele) akizungumza na wawakilishi wa kampuni mbalimbali zilizoomba zabuni kwa ajili ya mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme katika Maporomoko ya Maji ya Mto Rufiji kwenye ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam leo

MacAchayo aliongeza kuwa, katika awamu ya pili kampuni 17 zilijitokeza katika ununuzi wa nyaraka kwa gharama ya shilingi 500,000 kwa kila moja ambapo mpaka siku zinafunguliwa ni kampuni tano tu zimerejesha nyaraka zenye maombi ya zabuni.

Alisema hatua inayofanyika kwa sasa ni ufanyaji wa tathmini ya zabuni hizo na kusisitiza kuwa mara baada ya kukamilika kwa tathmini ya zabuni hizo waombaji wote watajulishwa mshindi na baada ya hapo zitafuata taratibu za mazungumzo, barua na kuandaa mkataba kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi mara moja.

Aliwataka kampuni zilizowasilisha maombi kuwa watulivu wakati zoezi la tathmini likiendelea.

 

101 thoughts on “Zabuni Mradi wa Umeme Rufiji zafunguliw

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama