Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wizara Yatoa Rai kwa Wadau wa Sekta ya Utalii Nchini Kuendeleza Programu ya Royal Tour, Yagawa Vifaa vya Kujikinga na Uviko – 19

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Francis Michael ameeleza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea kushirikiana vizuri na wadau wa Sekta ya Utalii katika kuendeleza Programu ya Royal Tour ili kuvutia watalii kutoka katika masoko mbalimbali duniani waje kutembelea vivutio vya utalii vya Tanzania.

Amesema Programu ya Royal Tour iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ni fursa ya Kimkakati ya kuitambulisha Tanzania Kimataifa,kuvutia uwekezaji nchini na kutangaza utalii.

Dkt. Francis Michael ameyasema hayo leo jijini Arusha alipokuwa akigawa vifaa vya kujikinga na janga la UVIKO- 19 kwa Wadau wa Sekta ya Utalii nchini.

17 thoughts on “Wizara Yatoa Rai kwa Wadau wa Sekta ya Utalii Nchini Kuendeleza Programu ya Royal Tour, Yagawa Vifaa vya Kujikinga na Uviko – 19

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama