Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wizara na Majeshi Wapitisha Mpango wa Muda Mfupi wa Michezo kwa Mashindano ya Kimataifa

Kamati ya Kitaifa ya kuendeleza michezo nchini inayojumuisha Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo, Baraza la Michezo la Majeshi Tanzania (BAMMATA), Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ) leo Oktoba 12, 2021 jijini Dar es Salaam wamepitisha mpango wa muda mfupi wa kuandaa  Timu za Michezo za Taifa  zitakazoshiriki  Michezo  ya Jumuiya ya madola nchini Uingereza mapema Julai hadi Agosti 2022.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Nasra Mohamed amesema tayari kamati yake imepitisha mpango huo hatua inayofuata ni kupeleka kwa Wizara yenye Sera na dhamana ya michezo nchini ili utekelezaji wake uanze mara moja kulingana na ratiba.

623 thoughts on “Wizara na Majeshi Wapitisha Mpango wa Muda Mfupi wa Michezo kwa Mashindano ya Kimataifa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama