Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri wa Maliasili Asisitiza Matumizi Bora ya Ardhi kwa Wananchi Wanaoishi Karibu na Maeneo ya Hifadhi

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amezitaka Halmashauri zote nchini ambazo zinapakana na maeneo ya hifadhi kupanga matumizi bora ya ardhi huku akiwataka wananchi kuacha kulima na kuanzisha makazi kwenye mapito ya wanyamapori.

Aidha, Waziri Dkt. Ndumbaro ameendelea kusisitiza kuwa wananchi wanatakiwa kuheshimu maeneo ya hifadhi huku akisisItiza kuwa  idadi ya tembo haijaongezeka kama inavyodaiwa badala yake idadi ya watu ndio imeongezeka 

Amesema kwa mujibu wa takwimu mwaka 1961 wakati nchi inavyopata uhuru idadi ya watu ilikuwa milioni nane huku idadi ya tembo nchi nzima ilikuwa 300,000 ambapo kwa sasa idadi ya watu imeongezeka hadi kufikia milioni 62 huku idadi ya tembo imepungua hadi kufikia 60,000

One thought on “Waziri wa Maliasili Asisitiza Matumizi Bora ya Ardhi kwa Wananchi Wanaoishi Karibu na Maeneo ya Hifadhi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama