Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Ndalichako: Serikali Inatambua Mchango wa Sekta Binafsi katika Kukuza Uchumi Nchini

Na: Mwandishi Wetu – Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan inathamini na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Sekta Binafsi katika ukuaji wa ajira na uchumi nchini. 

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 63 wa mwaka wa Chama cha Waajiri uliofanyika Jijini Dodoma tarehe Juni 22, 2022.
Amefafanua kuwa Sekta Binafsi ni msingi wa ukuaji wa ajira, na ni injini ya uchumi wa nchi yetu.

Mhe. Ndalichako, amefafanua kuwa sekta binafsi inatoa mchango mkubwa katika uzalishaji wa bidhaa na uwekezaji katika sekta za kimkamakati. Aidha, amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Waajiri wote hususani wa Sekta Binafsi katika kuibua fursa za maendeleo, kujadili changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi kwa haraka.

“Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ina imani kubwa na ATE na Waajiri wote katika kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini” amesema Mhe. Prof. Ndalichako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama