Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Ndalichako Awataka Vijana Kuchangamkia Fursa Zinazotolewa na Serikali

Na: Mwandishi Wetu – Kasulu, KIGOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amewataka vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi ili kuweza kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki zitakazowawezesha kumudu ushindani katika soko la ajira.

Mhe. Ndalichako ameyasema hayo Agosti 4, 2022 wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Nyamidaho VTC Kasulu, mkoani Kigoma kwa lengo la kukagua maendeleo ya wananufaika na programu ya Taifa ya kukuza ujuzi inayotekelezwa na Ofisi hiyo.

2 thoughts on “Waziri Ndalichako Awataka Vijana Kuchangamkia Fursa Zinazotolewa na Serikali

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama