Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Nape Afanya Mkutano wa Kutatua Mgogoro wa Anwani za Makazi Mbezi Jogoo

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye ameiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuanza mara moja zoezi la uwekaji anwani za makazi kwenye mtaa wa Jogoo uliopo katika Kata ya Mbezi Juu Jijini Dar es Salaam kufuatia kuwepo kwa mgogoro wa ardhi wa muda mrefu wa zaidi ya miaka 40 kwenye eneo hilo.

Eneo la Mtaa huo ambalo kabla ya Uhuru lilitengwa na Serikali kwa ajili ya kilimo cha mazao ya biashara, mwaka 1970 Rais Mstaafu wa Awamu ya Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Nyerere alilirudisha kwa wananchi na baadae kutengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda, kazi ambao haijafanyika ipasavyo ambapo kwa zaidi ya miaka 40 mpaka sasa, wananchi wamejenga makazi ya kudumu.

Katika mkutano wa pamoja kati ya Waziri Nape, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete, na Wakazi wa Mtaa huo, Waziri Nape ametoa agizo hilo kati ya maagizo sita ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu ya kutaka maeneo hayo yaendelee kuwa makazi ya kudumu ya watu na kupewa anwani za makazi huku waliokabidhiwa maeneo hao kwa ajili ya shughuli za viwanda na hawakuyaendeleza maeneo hayo, wachukuliwe hatua za kisheria.

One thought on “Waziri Nape Afanya Mkutano wa Kutatua Mgogoro wa Anwani za Makazi Mbezi Jogoo

 • May 16, 2022 at 1:28 am
  Permalink

  Соловьев обвинил свердловского сенатора Росселя в отсутствии патриотизма
  Владимир Соловьев в программе «России-1» обвинил свердловского сенатора Эдуарда Росселя в отсутствии патриотизма.
  Уральский меридиан
  Чуть раньше, общаясь на своём канале Соловьёв LIVE с полпредом президента в УрФО Владимиром Якушевым, журналист назвал Екатеринбург «центром мерзотной либероты».
  Царьград
  «Защита сенатором Росселем студенток, которые открыто высказались против знака «Z», наталкивает на мысль, что создание Уральской республики было не просто попыткой дестабилизировать Россию, а продуманным шагом», — сказал Соловьев.
  Общественная служба новостей
  Как заявил журналист в собственном шоу на канале «Россия», уральского политика самого «есть за что спросить» и призвал того «прийти в чувство».
  URA.Ru

  mega2226xhteoffdyiuyw6udqahbtepii7kwp6vn2y4cntm5llnnblqd onion

  megadmeovbj6ahqw3reuqu5gbg4meixha2js2in3ukymwkwjqqib6tqd.onion

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama