Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mwakyembe Azitaka Ofisi za Umma Kutoa Taarifa kwa Wanahabari

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na uongozi wa Arusha Press Club kuhusu namna bora ya kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Habari leo Jijini Dodoma.

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imezitaka ofisi za Umma kutoa taarifa kwa wanahabari kwa kuwa siyo hisani na siyo hiyari, bali ni takwa la kisheria kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 18 (d).

Kauli hiyo imetolewa na Waziri mwenye dhamana ya tasnia ya Habari Dkt. Harrison Mwakyembe alipokutana na ujumbe wa viongzi wa Chama cha Waandishi wa Habari kutoka mkoani Arusha pamoja na Asasi ya Vyombo vya Habari Mbadala (Alternative Media) leo jijini Dodoma.

“Serikali haina ugomvi na vyombo vya habari, bila vyombo vya habari hatutaweza kuwahabarisha wananachi masuala mbalimbali ya maendeleo ya nchi yetu” amesema Dkt. Mwakyembe.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akizungumza katika kikao cha Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na uongozi wa Arusha Press Club kuhusu namna bora ya kutekeleza majukumu yao ya kutoa habari sahihi kwa wananchi leo Jijini Dodoma.

Aidha, amewakumbusha wanahabari kuwa kazi wanayofanya ni muhimu sana ambapo nchi zilizoendelea bado wanatumia vyombo vyao vya habari ikiwemo Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ambalo lina miaka zaidi ya 90 na linatangaza habari zake kwa lugha zaidi ya 40 ili kuwafikia wananchi wake na dunia kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari kutoka mkoa wa Arusha Bw. Claud Gwandu amemshukuru Waziri Dkt. Mwakyembe kwa mapokezi, majadiliano yenye tija kwa uwazi na ukweli na kumpongeza kwa kazi nzuri anayofanya katika sekta anazozisimamia.

Mwenyekiti wa Arusha Press Club Bw. Claud Gwandu akizungumza jambo wakati wa kikao na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) ambapo walijadiliana masuala mbalimbali yanaohusu tasnia ya habari leo Jijini Dodoma.

“Tunamshukuru Waziri kwa kutupa nafasi ili tuweze kushirikiana katika kuimarisha tasnia ya habari iwe bora kwa mustakabali wanchi yetu” amesema Gwandu.

Aidha, Mwenyekiti huyo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayofanya kwa kutekeleza miradi mingi kwa manufaa ya Watanzania na kusisitiza kwa mwenye macho haambiwi tazama.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea kipeperushi cha majukumu ya uongozi wa Arusha Press Club mara baada ya kumaliza kikao na uongozi huo kuhusu namna bora ya kutekeleza majukumu yao ya kihabari leo Jijini Dodoma.

8 thoughts on “Waziri Mwakyembe Azitaka Ofisi za Umma Kutoa Taarifa kwa Wanahabari

 • August 10, 2020 at 3:48 pm
  Permalink

  I’ve learn a few good stuff here. Certainly price bookmarking for revisiting.

  I wonder how a lot attempt you set to make one of these magnificent
  informative web site.

  Reply
 • August 14, 2020 at 6:07 am
  Permalink

  Everything is very open with a precise description of the challenges.
  It was really informative. Your site is useful.
  Thank you for sharing!

  Reply
 • August 25, 2020 at 5:06 am
  Permalink

  Have you ever considered writing an ebook or guest authoring on other sites?
  I have a blog centered on the same subjects you discuss and would really like to
  have you share some stories/information. I know my audience would value
  your work. If you are even remotely interested, feel free to send me an e-mail.

  2CSYEon cheap flights

  Reply
 • August 28, 2020 at 12:20 am
  Permalink

  It is not my first time to visit this web page, i am browsing this site dailly and obtain pleasant facts from here all the time.

  Reply
 • August 28, 2020 at 9:56 am
  Permalink

  Hello, its fastidious piece of writing regarding media print, we all be familiar with media
  is a fantastic source of data.

  Reply
 • August 31, 2020 at 8:49 pm
  Permalink

  This piece of writing will assist the internet visitors for setting up new web site or even a blog from
  start to end.

  Reply
 • September 5, 2020 at 4:26 am
  Permalink

  Hi, its pleasant paragraph regarding media print, we all be familiar with media is a enormous source of information.

  Reply
 • September 5, 2020 at 1:44 pm
  Permalink

  I savor, lead to I discovered exactly what I was taking a look for.
  You’ve ended my four day long hunt! God Bless you man. Have a great day.

  Bye

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *