Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mwakyembe aongoza mapokezi ya Everton

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.  Harisson Mwakyembe akisalimiana na mchezaji Wayne Rooney wa timu ya Everton ya Uingereza  mara baada ya kikosi hicho kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.  Everton inatarajiwa kushuka dimbani kesho kwenye uwanja wa Taifa kumenyana na timu ya Gor Mahia ya Kenya mchezo ulioandaliwa na kampuni ya SportPesa.

Na. Mwandishi Wetu

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameongoza mapokezi ya timu ya Soka ya Everton ya Uingereza ambayo imewasili leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia kutoka Kenya.

Katika mapokezi hayo, Waziri Mwakyembe aliongozana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Bw. Yusuph Singo pamoja na wadau mbalimbali wa michezo ambapo timu hiyo kutoka Uingereza imeambatana na mchezaji nguli Wayne Rooney ambaye amesajiliwa kutoka timu ya Manchester United.

Kabla ya mchezo wake wa kesho, timu za Everton na Gor Mahia zinatarajiwa kufanya mkutano na Waandishi wa Habari leo majira ya alasiri katika uwanja wa Taifa.

Baadhi ya viongozi na wachezaji wa timu hiyo wakishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam asubuhi hii

Ujio wa Rooney na timu ya Everton unatarajiwa kuwa chachu katika maendeleo ya mpira wa miguu nchini na pia kuitangaza Tanzania kimataifa.

Mechi ya kesho kati ya Everton na Gor Mahia umeandaliwa na kampuni ya michezo ya Kubashiri nmatokeo ya SportsPesa ambayo ni miongoni mwa wadhamini wa timu ya Everton.

Kikosi cha timu ya Everton ya Uingereza kikiwa katika picha ya pamoja wakati kikishuka kwenye ndege iliyoileta timu hiyo kwenye uwanja wa Ndege wa JNIA jijini Dar es salaam.

Timu ya Gor Mahia ilipata nafasi ya kuchezaa mchezo huu baada ya kuwa mabingwa wa kombe maalumu lililoandaliwa na kampuni ya SportsPesa mbapo bingwa wa kombe hilo ndiye aliye pata nafasi ya kucheza na timu hiyo kutoka Uingereza.

 

130 thoughts on “Waziri Mwakyembe aongoza mapokezi ya Everton

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama