Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mwakyembe Akutana na Uongozi wa MISA –TAN Kujadili Maendeleo Katika Sekta ya Habari

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Uongozi wa Taasisi ya Habari ya MISA –TAN kuhusu maendeleo ya sekta ya Habari leo Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Habari ya MISA – TAN Bibi.Salome Kitomary (Kushoto) akitoa maelezo mafupi kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) wakati Taasisi hiyo ilipokutana nae leo Jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bw. Rodney Thadeus.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bw. Rodney Thadeus akimkaribisha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na MichezoDkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) kuzungumza na Uongozi wa Taasisi ya Habari ya MISA – TAN leo Jijini Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Habari ya MISA –TAN Wakili James Marenga akizungumza wakati wa kikao kati ya taasisi hiyo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na MichezoDkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) kuhusu maendeleo ya sekta ya Habari leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Taasisi ya Habari ya MISA –TAN pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara yake.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail