Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mkuu Majaliwa Afungua Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika Jijini Arusha

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akihutubia kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO), katika ukumbi wa AICC Arusha

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro, akikabidhiwa bendera ya Wenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO) kutoka wa Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi Sudan, Abdi Mohammed Bashir, kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa nchi hizo, katika ukumbi wa AICC Arusha,

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro, akipeperusha bendera ya Wenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO), baada ya kukabidhiwa Uenyekiti huo na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi Sudan, Abdi Mohammed Bashir, kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa nchi hizo, katika ukumbi wa mikutano wa AICC Arusha.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Sudan, Abdi Mohammed Bashir na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO) aliyemaliza muda wake, akizungumza, kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO), katika ukumbi wa AICC Arusha,

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipeana mkono na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Kongo DRC, kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO), uliyofanyika katika ukumbi wa AICC Arusha,

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipeana mkono na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro, baada ya kutoka kwenye ukumbi wa AICC Arusha, katika ufunguzi wa Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO) Septemba 19.2019

221 thoughts on “Waziri Mkuu Majaliwa Afungua Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika Jijini Arusha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama