Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mkuu Atoa Rai kwa Uongozi wa Chuo cha Ulinzi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa chuo cha Ulinzi cha Taifa uweke malengo endelevu yatakayokifanya kiwe kituo bora, bobezi, mahiri na chenye kutegemewa na Taifa katika masuala ya Ulinzi, usalama na mikakati.

Ametoa Wito huo Julai, 2021 katika mahafali ya tisa ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC), katika kozi ya usalama na mikakati, kilichopo Kunduchi mkoani Dar Es Salaam.

Amesema Serikali kwa upande wake itahakikisha kuwa chuo hicho Kinakuwa ni Kituo cha ufahari katika kutoa elimu ya juu kwa maafisa, watendaji kutoka vyombo vya ulinzi na usalama na watumishi wa umma.

Ameongeza kuwa anatambua na kuthamini mchango wa chuo hicho katika kutoa mafunzo yanayowajengea uwezo viongozi na watendaji mbalimbali kwenye masuala ya usalama na mikakati.

Hadi sasa maafisa waandamizi 300 kutoka vyombo vya ulinzi na usalama ndani na nje ya nchi na wengine kutoka katika taasisi za umma za kiraia wamenufaika na programu hii inayotolewa na chuo cha Taifa cha Ulinzi

Amesema kuwa chuo hiko kimeendelea kuwa sehemu muhimu katika kujenga na kuimarisha mahusiano ya mtu mmoja mmoja kwa washiriki wa program zake sanjari na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kimataifa kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

4 thoughts on “Waziri Mkuu Atoa Rai kwa Uongozi wa Chuo cha Ulinzi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama