Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mkuu Atoa Agizo Uendelezaji Zao la Mkonge

*Halmashauri zinazolima mkonge zatakiwa kuanzisha vitalu vya miche

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameziagiza Halmashauri zinazolima mkonge nchini pamoja na wakulima wakubwa wa mkonge watenge ekari 10 kwa akili ya kuanzisha vitalu vya kuzalisha miche ya mkonge ili kupunguza tatizo la upungufu wa mbegu.

Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Kilimo itenge fedha katika bajeti yake kwa ajili ya kituo cha TARI Mlingano ili kukiwezesha kupanua eneo la uzalishaji miche kwa kununua vitendea kazi yakiwemo matrekta.

Ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Januari 20, 2021) baada ya kukagua kitalu cha miche ya mkonge la TARI Mlingano lililopo wilayani Muheza, Tanga na kufungua zoezi la ugawaji wa miche kwa wakulima wa zao hilo.

Waziri Mkuu amesema ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa miche ya mkonge nchini kila halmashauri na wakulima wakubwa wanatakiwa watenge ekari 10 kwa ajili ya kuandaa vitalu vya miche ya mkonge na kugawa kwa wananchi kwenye maeneo yao.

One thought on “Waziri Mkuu Atoa Agizo Uendelezaji Zao la Mkonge

  • July 27, 2021 at 10:18 am
    Permalink

    Ahaa, its fastidious dialogue concerning this piece
    of writing here at this blog, I have read all that, so at this time me also commenting here.

    Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama